Imeboreshwa Dakika 50 zilizopita
Katika visiwa vya Norway katika Bahari ya Arctic kuna mji mdogo wenye wakazi 45 wakati wa majira ya baridi kali na hadi wakazi 150 kwenye kilele cha majira ya joto. Ni makazi ya kudumu ya kaskazini zaidi duniani, yaliyo karibu maili 765 (1,231km) kutoka Ncha ya Kaskazini.

Ny-Ålesund, ni mahali pazuri sana. Labda pia ni moja ya sehemu nzuri zaidi kwenye sayari ya kuvuta pumzi iliyo mbali na vyanzo vikuu vya uchafuzi wa mazingira katika mazingira ambayo hayajaguswa ya Arctic, hewa hapa ni safi zaidi dunaini.


Wakazi wa mji huo kwa kiasi kikubwa ni wanasayansi ambao huja kwa sababu hii. Mnamo 1989, kituo cha utafiti kilijengwa kwenye ubavu wa Zeppelinfjellet kwa mwinuko wa 472m (1,548ft) kusaidia watafiti kufuatilia uchafuzi wa anga. Hivi majuzi Kituo cha Uchunguzi cha Zeppelin, kama kituo cha utafiti kinavyoitwa, kimekuwa sehemu muhimu ya kupima viwango vya gesi chafuzi ambavyo vinasababisha mabadiliko ya hali ya hewa.

Lakini pia kuna ishara kwamba ubora wa hewa hapa unaweza kubadilika. Mara kwa mara mikondo ya anga hubeba hewa kutoka Ulaya na Amerika Kaskazini hadi sehemu hii ya Svalbard na kuleta uchafuzi kutoka kwenye maeneo hayo. Sio tu kwamba watafiti wanaona viwango vya uchafuzi fulani vinaongezeka, kuna dalili za aina mpya za uchafuzi unaofanywa kwenye upepo ambao unawatia wasiwasi wanasayansi.

"Kituo cha uchunguzi cha Zeppelin kiko katika mazingira ya mbali na safi, mbali na vyanzo vikuu vya uchafuzi wa mazingira," anasema Ove Hermansen, mwanasayansi mkuu katika Kituo cha Uchunguzi cha Zeppelin na Taasisi ya Utafiti wa Anga ya Norway. "Ikiwa unaweza kuipima hapa, unajua kwamba tayari ina maambukizi ya kimataifa. Hili ni eneo zuri la kujifunza mabadiliko ya anga."



Maelezo ya picha,
Watafiti lazima wachukue gari la kebo kutoka mjini ili kufikia chumba cha uchunguzi mlimani

Viwango vya methane angani karibu na Zeppelin, kwa mfano, vimekuwa vikiongezeka tangu mwaka wa 2005 na kufikia viwango vya rekodi katika 2019. Sasa kuna wasiwasi kwamba viwango vya uzalishaji wa methane unaosababishwa na binadamu vinatishia kupunguza kiwango cha ongezeko la joto duniani. 1.5C kupanda kwa joto.

Lakini sio habari mbaya kila wakati. Pia wameona viwango vya vyma vizito katika hewa kama vile risasi na zebaki vikipungua kwa kiasi kikubwa kutokana na kubana sheria za uchomaji taka na viwanda.

Juhudi za kupunguza matumizi ya viuatilifu vya organofosfati - ambavyo vinaweza kuingia hewani vinapopulizwa kwenye mashamba  pia vimeleta kupungua taratibu kwa kiasi cha kemikali hizi zilizogunduliwa katika angahewa karibu na Aktiki.


Maisha ya Ny-Ålesund
Cha kushangaza, haukuwa safi kila wakati. Kati ya 1916 na 1962, ulikuwa mji wa kuchimba makaa ya mawe, hadi mlipuko ulipotokea na kuua wachimbaji 21 na kusababisha mji huo kuhamishwa na mgodi kufungwa. Tangu wakati huo imebadilishwa kuwa mahali ambapo  hutolewa taarifa za kimazingira badala ya makaa ya mawe.

"Usafishaji umekuwa ukifanywa mara kwa mara tangu miaka ya 1960 wakati migodi ilipofungwa, lakini kwa bahati mbaya bado kuna uchafuzi wa mazingira ulioachwa katika eneo la migodi na katika jiji," anasema Hanne Karin Tollan, mshauri wa utafiti katika kituo cha Ny-Ålesund.

Lakini wakati wale wanaofanya kazi huko Ny-Ålesund wanatumia muda wao mwingi kuangalia juu ili kuona kile kilicho angani juu ya vichwa vyao, wakazi hao wanatoka sehemu mbalimba duniani ikiwa ni pamoja na Ufaransa, Ujerumani, Uingereza, Italia, Norway, Japan, Korea Kusini na China na sehemu nyingine.

Kuna safari mbili tu za ndege za kila wiki kwenda mjini kutoka Longyearbyen, Svalbard, ambazo hutolewa kwa ndege ya kupalilia-rattling.

Jiji lenyewe linajumuisha takriban majengo 30 yanayofanana na vibanda vya makabati yaliyopewa jina la miji mikubwa duniani kama Amsterdam, London, Mexico, Italia na mingine. Zinatumika kama ukumbusho wa hitaji la uhusiano wa kidiplomasia mahali hapa mbali na kukutana kwa watu.

Njia zingine za mawasiliano, hata hivyo, hazipatikani, simu zote za mkononi na Wi-Fi lazima zizimwe. Jiji ni eneo lisilo na redio ikiwa ni katika jaribio la kuweka mawimbi ya hewa katika eneo hilo kuwa kimya iwezekanavyo na ruhusa maalum inahitajika kwa watafiti ambao wanataka kuendesha kifaa chochote kinachotumia matangazo ya redio.


Ove Hermansen amechunguza uchafuzi wa hewa kwa zaidi ya miaka 20 katika kituo cha uchunguzi cha Zeppelin, ambapo watafiti lazima pia wawe makini na dubu

Miongoni mwa wale wanaotumia fursa ya anga safi na mazingira yasiyo na redio ni Mamlaka ya upimaji na ramani ya Norway, ambao wamejenga kituo cha redio cha mita 20 (65ft) ili kusaidia kufuatilia mienendo ya Dunia na sehemu zenye mvuto.

Dhoruba kali mara nyingi hupiga vibanda vya jiji, na usiku upepo huingia ndani.

Hali ya hewa kali ni hatari kwa wale wote wanaoishi na kufanya kazi hapa. Hali ya joto mara nyingi huwa chini ya baridi la kuganda na baridi kali kuwahi kurekodiwa ilikuwa -37.2C (-35F) wakati wa baridi. Machi mwaka huu hali ya joto ilifikia rekodi ya juu kwa mwezi ya 5.5C (42F). Rekodi ya awali kuwekwa ilikuwa ya 1976ya  5.0C (41F).

Unaweza kuona asili na hali kali pamoja na vipindi virefu vya giza au mwangaza wa jua.



Kuna hatari nyingine zaidi ya giza na baridi kwa watafiti wanaojitokeza wakati huu wa mwaka.

Svalbard ni makazi ya asili ya dubu (Polar bear) na kwa miaka mingi dubu walionekana karibu na makazi, hata wakiingia ndani. Kwa hiyo, jamii ina sheria kwamba hakuna mtu kufunga milango ya jengo lolote ili ikiwa dubu atatokea ndani ya makazi na ukahitaji msaada wa haraka itakusaidia kupata hifadhi.

"Lazima ubadilike na kufanya kazi karibu na dubu, na sio kinyume," anasema Christelle Guesnon, mmoja wa watafiti wanaofanya kazi katika Kituo cha Uchunguzi wa Zeppelin Norway.

"Dubu hupenda kufuata njia ya mto na mara nyingi hupita katika barabara kati ya makazi ya Ny-Ålesund na kituo cha uchunguzi cha Zeppelin. Mara nyingi ukweli ni kwamba tunaweza kuwa kwenye chumba cha uchunguzi na dubu akaingia, Kisha tunasubiri hadi aondoke."

Saa kumi na nusu jioni 16:30 ndio mwisho wa siku ya kazi, jumuiya ndogo huelekea ndani ya nyumba.

Kutokuwa na mawasiliano ya hapo na mawasiliano ya simu za mkononi kunamaanisha hutegemea mipango iliyofanywa mapema siku hiyo kwa mawasiliano yoyote.

Mgahawa wa jiji ni mahali pekee ambapo watu hukutana ili kujumuika wakati wa chakula cha mchana na chakula cha jioni, wakibadilishana mawazo kuhusu Taa za Kaskazini na wanyamapori waliokutana nao.

Leif-Arild Hahjem, ambaye amefanya kazi kwa miaka mingi huko Ny-Ålesund kama mhandisi anasema kuwa amekuwa katika eneo hilo tangu 1984 na ameona mabadiliko makubwa katika mazingira yanayomzunguka.


"Fjord iliyo karibu na makazi iliganda wakati huo, unaweza kwenda na gari la theluji lakini tangu 2006/7 haijawahi kuganda tena," anasema. "Makazi hayo yamezungukwa na barafu nyingi ambazo zote zinapungua inatokana na kuongezeka kwa joto."

"Leo, tunapitia athari za Arctic yenye joto katika maeneo kadhaa," anasema. "Kwa mfano, kuongezeka kwa maji ya joto ya Atlantiki ambayo hubadilisha mfumo mzima wa ikolojia katika fjord nje kidogo ya Ny-Ålesund, Inaathiri hata dubu ambao wanalazimika kurekebisha mlo wao. Sasa tunaona ongezeko kubwa la dubu wanaotafuna mayai kutoka kwenye viota vya ndege wa baharini."

Katika anga na mandhari, wakaazi wa Ny-Ålesund wanashuhudia alama mahususi za mabadiliko ya ulimwengu wetu kwa ujumla. Kwa sasa, hata hivyo, bado wanaweza kuvuta hewa wakijua kwamba hewa wanayovuta ni rasilimali adimu na ya thamani.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/rawegKD
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI