Jonas Mkude Kuweka Rekodi Mpya Simba SC



KIUNGO mkabaji wa Simba, Jonas Mkude amesema anafurahi kuendelea kuweka rekodi ya kuwa mchezaji anayeshiriki matamasha mengi ya Simba Day ndani ya timu hiyo.


Mkude amefunguka hayo kuelekea siku ya Simba Day inayotarajiwa kufanyika Agosti 8 mwaka huu, Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.


Kupitia mtandao wa kijamii Instagram ameandika kuwa ‘Agosti 8 tunaadhimisha Simba Day ya 14 kwangu mimi binafsi ni ya 12,”


“Ni heshima kwangu kuwa sehemu ya tamasha hilo kubwa la soka kwa miaka yote hiyo, tukutane kwa Mkapa kuadhimisha siku yetu wanasimba,” ameandika Mkude.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/m4fS0D1
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI