Kibwana Shomari wa Yanga Atetemeka Baada ya Kuona Uwezo Mkubwa wa Lomalisa...Atangaza Kumwendea Uluguru

 


Beki wa Yanga, Kibwana Shomari ni kama ametangaza vita baada ya kusema hana wasiwasi na ujio wa beki Joyce Lomalisa kwenye kikosi hicho.

Kibwana mwenye uwezo wa kucheza beki wa kulia na kushoto, msimu uliopita alicheza zaidi kushoto na kuwaweka benchi Yassin Mustapha na David Bryson ambao baadaye walikuwa wanasumbuliwa na majeraha.


Ujio wa Lomalisa unatishia uwezekanao wa Kibwana kupata namba lakini ametamka kwamba kila mmoja atumie vizuri nafasi anayopewa.


“Ni kitu kizuri kuja kwake kwenye timu, mimi nikipata nafasi nitaonyesha nilichonacho ili kuisaidia timu kufanya vizuri,” alisema Kibwana na kuongeza;


“Kweli wameimarisha eneo hilo na lengo ni timu kupata mafanikio na hilo sio suala geni kwenye mpira kwani mtu kutoka sehemu moja kwenda nyingine ni kawaida.”


Kuhusu kucheza nafasi mbili tofauti alisema; “Kama mchezaji unatakiwa unapopewa nafasi tofauti na uliyozoea basi unatakiwa kumsikiliza kocha nini anakuambia na ufuate maelekezo, naamini nilifuata maelekezo ndio maana nikawa nacheza.”



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Pg5MzF3
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI