Linah Sanga Afunguka Mapenzi na Mume wa Nandy Bilnass "Hatuna Uadui"

 


Kumekuwa na maneno mengi na watu wakijiuliza Linah alipata wapi ujasiri wa kuhudhuria harusi ya Billnas na Nandy wakati amewahi kuwa kwenye mahusiano na Nenga, haikuishia hapo, bado watu wanashangaa kuona Linah bado yupo karibu na familia hiyo kiasi kwamba hadi kwenye Nandy Festival alikuwepo, huku wengi wakihofia kuwa upashaji kipolo hauhitaji moto mwingi, na yeye ni binadamu ambaye ustahimilivu wa kuendelea kuwasiliana na Ex wako bila madhara inahitaji imani sana.😀


Hasa kupitia Amplifaya ya Clouds Fm, Linah amesikika akisema uEX sio uadui, kuachana na mtu si lazima mugombane au ndio uwe mwisho ya kuongea, kuna maisha mengine lazima yaendelee. Linah pia amedai maneno haya yamekuwa yakiendelea mitandaoni hayaleti picha nzuri kwake hata kwa wananfoa na yanakuzwa sana, kuna muda ataongea hili kwa undani zaidi.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/mtFZpEf
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI