Roma Mkatoliki "Msimsimange Mwanangu Mandonga BADO Nina Imani na Yeye"


Kufuatia Pambano la Bondia Karim Mandonga usiku wa kuamkia leo, kupigwa kwa TKO Round ya 4 dhidi ya mpinzani wake Bondia Shaban Kaoneka, rappa Roma ambaye ni shabiki wa Mandonga ameeleza haya machache kuhusiana na Mandonga kupoteza pambano lake.


Roma ameeleza Mandonga asisimangwe, bado ana Imani nae, akitolea mfano wa pambano la Bondia mkongwe Mike Tyson na Buster Douglas, katika pambano la mwaka 1990.


"Tarehe 11, February Mwaka 1990, #BusterDouglas Alimpiga K.O #Tyson Na Mike Akashindwa Kuendelea Na Pambano!! Swala La Kupigwa Kwenye Mchezo Wa #Vitasa Ni La Kawaida Sana. So Msimsimange Mwanetu #Ndonga “BADO NINA IMANI NA YEYE” - Ameeleza Roma kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.


Fahamu, hili ni pambano la pili mfululizo kwa Bondia Karim Mandonga kupoteza kwa TKO.


Je wewe bado una Imani na #Mandonga 🤔




from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/bVrSqAK
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI