Unamjua Vizuri Idd Amin wa Uganda? Soma Mambo Haya 10 Ubaki Mdomo Wazi..!!!



1.Aliwahi kuwa bingwa wa ndondi wa uzito wa juu nchini Uganda mwaka 1960-1961

2.alijichagua kuwa Raisi wa Uganda kwa mapinduzi ya kijeshi, na waganda wengi walimchukulia kuwa ni shujaa kwa kumuondoa raisi walieona “anasuasua” Milton Obote mwaka 1971.

3.Aliua watu zaidi ya laki tatu (300,000) kwa kipindi cha miaka 8 aliyokuwepo madarakani kabla ya Kung’olewa na Majeshi ya kitanzania mwaka 1979 baada ya kutaka kuteka sehemu ya Tanzania.

4.Aliwatimua raia wote wenye asili ya Kihindi nchini kwake na kutaifisha mali zao zote.

5.alijipa vyeo kibao na kujiita Field Marshall Al Hadj Doctor Idi Amin Dada!

6.Inasemekana alimtumia malkia wa uingereza Elizibeth II barua za kimapenzi akimuomba amuoe ili aweze kujiita mfalme kwani alikuwa ameshajipa vyeo vyote kasoro “King” Yaani mfalme.

7.Ana watoto zaidi ya 40 huku akiwa ameoa wake 6. Mmoja wa wake zake alikutwa ameuawa kinyama baada ya kupata ujauzito na mtu mwingine.

8.Vyombo kadhaa vya Habari vimekuwa vikimuhusisha na ulaji wa nyama za watu hasa maadui zake aliowaua.

9.Licha ya Ukatili dhidi ya binadamu, Idi amin hajawahi kufikishwa mahakaman mpaka anakufa mwaka 2003 na kuzikwa nchini Saudi Arabia alikokuwa akiishi uhamishoni.

10. Aliwahi kutua Nairobi kwa dharula na akiwa na mahusiano mabaya na nchi ya Kenya,
Ndege yake ilibainika kuwa na hitilafu serikali ya Kenya ilimpatia Ndege ya Polisi ili imfikishe Kampala lakini Alikataa kuhofiwa kutungulia hivyo kupelekea Makamu wa Rais wa kenya kupanda nae mpaka Kampala

from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/wajor4v
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI