Rais Samia ataja sababu ya Jeshi la Polisi kuwa legelege


 By Florah Temba

Moshi. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema upungufu wa mafunzo ndani ya Jeshi la Polisi ndio unaolifanya jeshi hilo kulegalega.


 Rais Samia ameyasema hayo leo Jumanne Agosti 30, 2022 wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha maofisa wakuu waandamizi wa polisi makao makuu, makamanda wa polisi wa mikoa na vikosi kinachofanyika katika ukumbi wa Shule ya Polisi Tanzania (TPS) mkoani Kilimanjaro.


"Tathmini yetu ni kwamba upungufu wa mafunzo ndio unalolifanya Jeshi la Polisi maeneo mengine liwe limelegalega au kuwepo na mmomonyoko wa maadili ndani ya jeshi," amesema Rais Samia.


"Inaweza ikiwa factor (sababu) ni ajira, nepotism nani kamwajiri nani, mlete tuu hivyo hivyo lakini huko nyuma niliwahi kuuliza huko chuoni ni wangapi wanashidwa nikaambiwa aah watu huko wanakwenda tu lakini nashukuru hawa waliohitimu juzi wapo walioshindwa,


"Nataka niwaambie hawa watu wasiposhindwa twendeni tu.... ni wale ambao wanaenda kulitia Jeshi la Polisi aibu, wanalolifanyia fedheha kwenda kufanya mambo ya ajabu ajabu wanapigwa picha wanarushwa kwenye mitandao vitendo vya ajabu ajabu ni kwasababu hawana maadili," amesema Rais Samia na kuongeza


Amesema kuwa hali hiyo ya ukosefu wa mafunzo ya mara kwa mara inachangia baadhi polisi kutokuwa na nidhamu.


ADVERTISEMENT

"Ndio maana unakuta polisi "in uniform" anausifia ulevi na anajipa ina zuri la kiingereza, nadhani upungufu wa mafunzo ndio haya matokeo yake.


"Kuanzia mwaka huu tumetoa fedha nyingi kwa ajili ya mafunzo, tumetoa Sh11 bilioni zikafunishe askari wetu wawe waadilifu wafuate maadili hiyo ndio kazi waliyoichagua na kama mtu anaingia polisi kama amekosa kazi sehemu nyingine basi tuchujane na tuone jinsi tunavyokwenda," amesema.


Kuhusu mfuko wa kufa na kuzikana katika jeshi hilo, Rais Samia amesema yapo matumizi mabaya ya fedha za askari za mfuko huo na kwamba fedha hizo askari anapofiwa hapewi licha ya michango kufanyika.


"Huu mfuko ni nguvu za askari, mfuko wa kufa na kuzikana, fedha zinakaa kwenye akaunti za jeshi lakini matumizi yanapofanywa askari hawana taarifa, ripoti za fedha hakuna, nilikuwa naongea na CAG hapa akanambia ameombwa kufanya ukaguzi maalumu maana ushirikiano kwa wale wanaofiwa hakuna.


"Kama mfuko ni wa kufa na kuzikana basi watu wapewe wanapofiwa na hiyo fedha itoke, lakini unakuta fedha zinatoka na askari wanafiwa na  hawafaidiki na wanaofaidika ni wachache lakini ukienda kutizama fedha zilizochangwa hazipo zimetumikaje haieleweki," amesema Rais Samia



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/cIXzFZB
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI