TBS yateketeza vipodozi vya Milioni 100




SHIRIKA la Viwango (TBS) Kanda ya kati limeteketeza Vipodozi na bidhaa za Vyakula zilizoisha Muda tani 31.2 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 100 katika Dampo la Chidaya jijini Dodoma.

BIDHAA mbalimbali za vyakula na vipodozi vyenye thamani takribani ya shilingi za Kitanzania milioni 7 zimeteketezwa katika dampo la Manispaa ya Mpanda baada ya kukutwa hazikidhi viwango kwa mujibu sheria ya Viwango Na 2 Sura 130.

imeteketeza vipodozi na bidhaa za vyakula zilizoisha muda  tani 31.2 zenye thamani ya

Hayo yameelezwa leo Agosti 26,2022 jijini Dodoma na Mkaguzi wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Kati Domisiano Rutahala wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika dampo la Chidaya ambako ndiko bidhaa hizo  na vipodozi  vimeteketezwa.

Bidhaa na vipodozi zilizoteketezwa ni kutoka katika Mikoa ya Dodoma,Singida na Tabora na ni  kuanzia Novemba 2021 hadi Agosti 2022.

Mtaalamu huyo amesema bidhaa zilizoteketezwa ni zile zilioisha muda pamoja na vipodozi vyenye viambata vya sumu na vilivyoisha muda wake.

“Kwa ujumla bidhaa zote ni tani 31.2 sawa na  kilo 3200 zenye thamani ya shilingi  milioni 100.9,”amesema Mtaalamu huyo kutoka TBS

Amesema wanateketeza bidhaa hizo kutokana na kuwa na madhara makubwa katika mwili wa mwanadamu.

“Bidhaa za chakula ambazo zimeisha matumizi zina athari kubwa sana mojawapo kutopatikana kwa virutubisho vinavyohitajika pia zinasababisha magonjwa ya muda mrefu na mfupi kama Saratani.

Kwa upande wa vipodozi vinaathari kubwa sana kiuchumi na madhara  ya muda mfupi na mrefu kuathiri mifumo ya macho,ukuaji wa watoto na kina mama wajawazito,”amesema Mtaalamu huyo

Hata hivyo  anawaasa wafanyabiashara wote kuwa makini kwa kufanya ukaguzi wa bidhaa zao na wajiepushe na uuzaji wa bidhaa zenye viambata vya  sumu kwani vina madhara makubwa

Aidha,wanawaomba wazingatie maelekezo ya utunzaji wa bidhaa hizo ili kuendana na uzalisha pamoja na kulinda ubora wake.

Kwa upande wa  wananchi,Bw.Rutahala amewaomba  waepuke kutumia bidhaa zenye viambata vyenye sumu  na kufanya ukaguzi wa kuangalia  mwisho wa matumizi ili kuepuka madhara.

“Wafanyabiashara  tunapowakamata tuna hatua mbalimbali ambazo huwa tunazichukua zimetaja aina ya faini na hatua za kuchukua,ikiwa ni pamoja na kuzichukua bidhaa hizo na kwenda kuzitekeleteza,”amesema.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/K8Q0qwp
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI