Tukio la Rayvanny Kumzawadia Gari Producer s2kizzy Hakijamzuia Producer Huyo Kushusha Ngoma za Rayvanny Youtube...Kunani?


Kitendo cha s2kizzy kushusha nyimbo za Mama Tetema kwenye mtandao wa YouTube, Rayvanny ft Diamond Platnumz na ile ya Maluma Ft Rayvanny, kimewaudhi wengi na S2kizzy akionekana ni mtu ambaye ana kinyongo na Rayvanny, na kinacho waumiza akili watu, ni kwanini anayafanya yote haya baada ya Rayvanny kuondoka WCB.


May 10, 2019 Rayvanny alimzawadia gari producer s2kizzy aina ya Mark X kama zawadi yake ya birthday ambapo producer huyo usherehekea siku yake ya kuzaliwa kila ifikapo May 9 kila mwaka. Akiwa kwenye kipindi cha Block 89 cha Wasafi Fm, S2kizzy alifanyiwa suprise na Rayvanny akiwa na ufunguo wa gari. Kikubwa Rayvvany alidai amefanya hivyo kama sehemu ya kushukuru mchango wa producer huyo kwa kumtengenezea ngoma nyingi ambazo zimekuwa ni pendwa ,ikiwemo Mama Tetema ambayo ilikuwa na miezi mitatu tu, toka itoke February 7,2019.


Kingine kilicho msukuma zaidi Rayvanny kufanya hivyo, ni baada ya kuona S2kizzy anasumbuka kuhusu usafiri, muda mwingine kupanda bajaji anapowahi sessions n.k, S2kizzy ambaye alimwaga chozi la furaha hadharani, aliahidi kuwa ndugu wa Rayvanny maisha yake yote, ikumbukwe gari ilikuwa nje na mikataba yao ya kufanya kazi kama producer na msanii.


Ni kweli ndugu ugombana, ila kwa hili, linazua picha kubwa na mbaya kati ya hawa wawili, japo hakuna hata mmoja kati yao amewahi liongea kwa kina hili, mbali na S2kizzy kukana kuwa sio yeye, japo jina lake kwenye claims linaonekana.


Throwback Thursday.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/dJhbvFr
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI