William Ruto Ataka Kesi Iliyowasilishwa Mahakama ya Juu Kupinga Ushindi Wake Ifutiliwe Mbali



William Ruto amewasilisha majibu yake kwenye kesi iliyowasilishwa na Raila Odinga wa Azimio katika Mahakama ya Juu, kupinga ushindi wake kwenye uchaguzi wa Agosti 9
Kwenye majibu hayo ya kurasa 256, Ruto anaitaka Mahakama hiyo kutupilia mbali kesi iliyowasilishwa na Raila kwa sababu anataka handshake ili akabidhiwe mgao wa serikali
Ruto ameongeza kusema kwamba Raila ana rekodi za kupinga kila matokeo ya uchaguzi mkuu, kiasi cha kulazimisha maelewano yatakayomwezesha kupata sehemu ya serikali
Rais mteule William Ruto amewasilisha majibu yake kwenye kesi iliyowasilishwa na Raila Odinga wa Azimio katika Mahakama ya Juu, kupinga ushindi wake kwenye uchaguzi wa Agosti 9.

William Ruto Ataka Kesi Iliyowasilishwa Mahakama ya Juu Kupinga Ushindi Wake Ifutiliwe Mbali
Naibu Rais William Ruto. Picha: UGC.
Kwenye majibu hayo ya kurasa 256, Ruto anaitaka Mahakama hiyo kutupilia mbali kesi iliyowasilishwa na Raila kwa sababu anataka handshake ili akabidhiwe mgao wa serikali.

Ruto ameongeza kusema kwamba Raila ana rekodi za kupinga kila matokeo ya uchaguzi mkuu, kiasi cha kulazimisha maelewano yatakayomwezesha kupata sehemu ya serikali.

Azimo Yataka Kesi Zilizowasilishwa na Moses Kuria, Reuben Kigame Kuondolewa Katika Mahakama ya Juu
Ruto alitoa mfano wa serikali ya nusu mkate iliyoundwa baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007, enzi za Mwai Kibaki na ya punde mwaka wa 2017 waliposalimiana na Rais anayeondoka Uhuru Kenyatta.


“Hulka ya kwanza inayojulikana ni kwamba kwa kipindi cha miaka 30 amekuwa akipinga matokeo ya uchaguzi mkuu na kukimbia mahakamani baada ya uchaguzi wa urais kutangazwa.

Hatua yake imeonekana ni juhudi za kumlazimisha mshindi wa urais kumgawanyia mamlaka kupitia njia zisizotambulika kwa mujibu wa katiba almaarufu handshake,” Ruto alisema siku ya Ijumaa, kwenye majibu ya kesi hiyo kupitia mawakili wake.

Kwenye kesi aliyowasilisha katika mahakama hiyo, Raila anataka ushindi wa Ruto ubatilishwe, kwa kusema kwamba hakushinda kihalali kwa kuwa Tume ya IEBC, ilisimamia uchaguzi uliogubikwa na ulaghai.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/to5JTHv
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI