Bodi ya Filamu nchini Kenya Yazifungia Filamu Zenye Maudhui ya Mapenzi ya Jinsia Moja


Bodi ya Filamu nchini Kenya, The Kenya Film Classification Board (KFCB) imezifungia filamu zote nchini humo zenye maudhui ya mapenzi ya jinsia moja, (Ushoga/Usaganaji n.k) kama maudhui ambayo yapo kinyume na sheria za nchi.

Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Christopher Wambua akiwa kwenye moja ya kituo cha radio nchini humo alipokuwa akifanya Interview siku ya jana ijumaa September 23, alidai bodi itaendelea kufungia na kutoruhusu contents hizo nchini humo hata kama wanachuja filamu kulingana na umri wa watazamaji, lakini bado haiondoi kuwa kuna mambo sheria za nchi haziruhusu. Wambua pia amedai hilo haliishii kwenye Media za Kenya tu (Mainstream) wapo kwenye mazungumzo na mitandao inayotumika kuonyesha filamu kama Netflix, kuzuia Maudhui ya aina hiyo kuonekana nchini humo.

“I am Samuel ” ni moja ya filamu iliyokula nyundo hivi karibuni nchini humo ikiwa na maudhui ya aina hiyo.

NB: Picha zilizotumika ni waigizaji wa Kenya pamoja na CEO wa KFCB, hazihusiani moja kwa moja na taarifa ya utengenezaji wa maudhui ya mapenzi ya jinsia Moja.




from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/h6u13ZE
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story