CEO mpya aipa jeuri Yanga kuitoa Al Hilal




ZIKIWA zimebaki takriban siku 11 kabla ya Yanga kuikaribisha Al Hilal kwenye mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika,...

... uongozi wa klabu hiyo umemtambulisha rasmi Mtendaji wao Mkuu (CEO), Mzambia Andre Mtine, ambaye wameingia naye mkataba wa miaka miwili akichukuwa nafasi ya Senzo Mbatha aliyemaliza 'kandarasi' yake hivi karibuni.

Mtine amewahi kufanya kazi katika klabu mbalimbali hapa Afrika ikiwamo Zesco ya kwao Zambia, TP Mazembe ya DR Congo na kuhudumu katika Shirikisho la Soka Afrika (CAF) katika kitengo cha fedha.

Yanga sasa inajivunia uzoefu CEO huyo ambaye anamjua vema Kocha Mkuu wa Al Hilal ya Sudan wa sasa, Florent Ibenge, tangu akiwa anafanya kazi nchini Congo kabla ya wote kuondoka.

Tayari imeelezwa Mtine ameanza kushusha hesabu zote zitakazoisaidia Yanga kuwashangaza matajiri hao wa Sudan, ikiwamo mikakati ya kocha wa timu hiyo, Ibenge ambaye ni raia wa DR Congo.


Kutokana na uzoefu na kufahamu uwezo wa Mtine katika soka, mabosi wa Yanga wameshaanza kuchukua tahadhari na hesabu zote na CEO huyo kuzingatia mechi mbili ili kupata matokeo chanya dhidi ya Al Hilal.

Yanga itaanzia nyumbani dhidi ya Al Hilal Oktoba 8, mwaka huu, kabla ya timu hizo kurudiana baada ya wiki moja nchini Sudan, na mshindi wa jumla atatinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza na gazeti hili jana, Rais wa Yanga, Hesri Said, alisema kwa uzoefu wa Mtine, anaamini timu yao itafikia malengo makubwa katika mipango yao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wakianza dhidi ya Al Hilal ya Sudan.


Alisema baada ya mchakato wa kupitia maombi ya waliomba kazi, Mtine amekidhi vigezo kwa sababu ya kuhudumu kufanya kazi sehemu mbalimbali katika soka la Afrika.

"Tumempa mkataba wa miaka miwili na kumtambulisha Mtine, tunaimani na uzoefu wake kwa kuhudumu katika nchini mbalimbali za soka ikiwamo CAF, atatusaidia kufikia malengo na Yanga kufika mbalimbali katika michuano ya Afrika.

"Kwa sasa tunakabiliwa na mchezo wa kimataifa, kwa uzoefu wake tunaimani tutapiga hatua katika mechi hizo na michuano ya Afrika ambayo Yanga tuna malengo makubwa," alisema Hersi.

Naye Mtine alisema anafurahi kufanya kazi Yanga kwa sababu ni klabu kubwa na atahakikisha kwa ushirikiano mkubwa wa uongozi watafikia malengo yanayotarajiwa.

Alisema ana uzoefu mkubwa katika utendaji na kufahamu soka la Afrika jambo ambalo litasaidia katika kuifikisha klabu hiyo katika malengo yanayotarajiwa.

"Nimefurahi kuja Tanzania na kufanya kazi Yanga katika klabu kubwa, ninaimani kwa ushirikiano na viongozi na sekta mbalimbali katika uongozi wa klabu hii, tutafikia malengo yanayotarajiwa kwa klabu kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa, ikiwamo kupata matokeo mazuri katika michezo iliyopo mbele yetu," alisema Mtine.

Wakati huo huo, Yanga imetambulisha mfumo mpya wa website, App ambao utawasaidia wanachama na mashabiki kupata nafasi ya kujisajili, lakini pia kupata taarifa za klabu yao.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Tb6QqYn
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI