Vita vya Ukraine: Je, Urusi Itatumia silaha za kimbinu za Nyuklia?



Rais wa Urusi Vladmir Putin amesema yuko tayari kutumia silaha za nyuklia kutetea ardhi ya Urusi, na hivyo kuzua hofu kuwa huenda akatumia silaha ndogo ya nyuklia nchini Ukraine.

Rais wa Marekani Joe Biden amemuonya kuwa kufanya hivyo kutakuwa ni ongezeko kubwa la mzozo kijeshi tangu Vita vya Pili vya Dunia.

Silaha za kimbinu za nyuklia ni za aina gani?

Silaha hizi za nyuklia ni silaha na mifumo yao ya uwasilishaji kwa matumizi ya kwenye uwanja wa vita au kwa mgomo mdogo.

Silaha za hizi za nyuklia zimeundwa kuharibu malengo ya adui katika eneo maalum bila kusababisha uchafuzi wa mionzi.

Silaha ndogo zaidi za nyuklia zinaweza kuwa tani elfu moja au chini ya hapo, ambayo ni, tani elfu moja za mlipuko wa TNT, na kubwa zaidi inaweza kufikia tani laki moja za mlipuko wa TNT.

Silaha za kimkakati za nyuklia ni kubwa (hadi daraja la megaton) na zinaweza kurushwa kutoka umbali mkubwa zaidi.

Kwa kulinganisha, bomu la atomiki lililorushwa na Marekani huko Hiroshima mnamo 1945 lilikuwa tani 15,000.

Aina gani ya silaha za kimbinu ilizonazo Urusi?
silaha
Kwa mujibu wa idara ya ujasusi ya Marekani, Urusi ina takribani silaha za nyuklia za 2,000.

Vita vya nyuklia vya kimbinu vya Urusi vinaweza kuwekwa kwenye aina mbalimbali za makombora ambayo mara nyingi hutumiwa kutoa vilipuzi vya kawaida, kama vile makombora ya masafa.

Silaha za kimkakati za nyuklia pia zinaweza kurushwa kutoka kwenye ndege au meli - kama makombora ya kuzuia meli, torpedo. Urusi hivi karibuni imekuwa ikiwekeza sana katika silaha hizi, Marekani ilisema.

Je, silaha za kimbinu za nyuklia ziliwahi kutumika hapo awali?
silaha
Chanzo cha picha, Getty Images

Silaha za nyuklia za kimkakati hazijawahi kutumika katika migogoro.

Mataifa yenye nguvu za nyuklia kama vile Marekani na Urusi yameona inafaa kutumia zana za kisasa za kivita kuharibu shabaha kwenye medani ya vita.

Zaidi ya hayo, hadi sasa, hakuna serikali iliyo tayari kusababisha vita kamili vya nyuklia kwa kutumia silaha za mbinu za nyuklia.

Hatahivyo, Urusi inaweza kupendelea kutumia silaha ndogo kuliko silaha kubwa za kimkakati. "Pengine hawafikirii kuwa wanavuka eneo hili kubwa la nyuklia," alisema Patricia Lewis, mkuu wa Mpango wa Kimataifa wa Usalama katika Chatham House. "Wao (Urusi) wanaweza kuiona kama sehemu ya vikosi vyake vya kawaida."

Je, tishio la nyuklia la Putin kweli linaleta hofu?
Mnamo Februari 2022, muda mfupi kabla ya uvamizi wa Ukraine, Rais Vladimir Putin aliweka vikosi vya nyuklia vya Urusi kwenye "utayari wa kupambana" na kufanya mazoezi ya kiwango cha juu.

Hivi majuzi, alisema, "Ikiwa eneo la nchi yetu linatishiwa, tutatumia njia zote zinazopatikana kulinda Urusi na watu wetu bila shaka.”

Urusi inapanga kura ya maoni isiyotambulika kimataifa kutwaa maeneo ya kusini na mashariki mwa Ukraine baada ya kuteka maeneo ya kusini na mashariki.

Lakini pia kuna wasiwasi kwamba ikiwa Urusi inakabiliwa na vikwazo zaidi, inaweza kujaribiwa kutumia silaha ndogo za kimbinu nchini Ukraine.

"Nina sababu ya kuwa na wasiwasi kwamba, katika hali hiyo, Putin anaweza kutumia silaha za nyuklia -- pengine ndani ya Ukraine, kutisha," alisema James Acton, mtaalam wa nyuklia wa Shirika la Carnegie Endowment for International Peace huko Washington.

Rais wa Marekani Joe Biden ameionya Urusi dhidi ya kutumia silaha za nyuklia katika vita vya Ukraine.

Katika mahojiano na CBS News , Biden alisema hatua kama hiyo "itabadilisha mchezo wa vita tofauti na kitu chochote tangu Vita vya pili vya dunia," na kuongeza kuwa "kutakuwa na athari mbaya."

Iwapo silaha zozote za nyuklia zitatumika, ni vigumu kutabiri jinsi Marekani na NATO zitakavyojibu.

Huenda hawataki kuhatarisha vita kamili vya nyuklia na kuzidisha hali hiyo zaidi, lakini pia wanaweza kutaka kuchora mstari.

Hata hivyo, Urusi inaweza pia kuzuiwa kutumia silaha za nyuklia za kimbinu na nguvu nyingine kubwa.

"Urusi inategemea sana msaada wa China," alisema Heather Williams, mtaalamu wa nyuklia katika Chuo cha King's College London. "Lakini China ina kanuni ya kutotumia silaha hizo. Hivyo kama Putin atatumia silaha za nyuklia, itakuwa vigumu kwa China kumuunga mkono." "Ikiwa atazitumia (silaha za nyuklia), anaweza kupoteza (msaada) kutoka China."




from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/6cvqoQB
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI