Mbagala kupelekewa mabasi 750 ya mwendokasi



Dar es Salaam. Mabasi 750 Yaendayo Haraka yanatarajiwa kuanza kufanya kazi katika barabara ya Mbagala jijini Dar es Salaam, Machi 2023.

Hayo yamesemwa leo Jumamosi Oktoba 29, 2022 na Mkurugenzi wa Maendeleo ya  Usafirishaji wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), Fanuel Karugendo walipojumuika na wakazi wa Mbagala na wadau wengine kufanya usafi katika Kata ya Mbagala.

Karugendo amesema mradi huo ambao ni awamu ya pili unatarajiwa kuanza na mabasi 750 kutokana na wingi wa watu katika eneo hilo.

 Aidha Mkurugenzi huyo amesema mradi huo utasaidia kusafirisha abiria 600,000 mpaka 700,000 kwa siku kupitia barabara hiyo.

"Hata katika kuja kushiriki usafi leo ni katika kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kujiandaa na ujio wa mabasi hayo ambayo asili yake ni kutoa huduma katika mazingira safi,"amesema Karugendo.

Mkazi wa eneo hilo, Shukuru Othuman amesema usafiri huo utamaliza changamoto zao za usafiri wa umma katika eneo hilo.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/12YnOPC
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI