Tanzania Yafikisha Watu Milioni 61.74

.


Dodoma. Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika Agosti, akisema kuwa idadi ya watanzania ni milioni 61.74.

Amesema hayo leo Jumatatu Oktoba 31, 2022 kati ya hao Watanzania milioni 59.8 wako Tanzania Bara na watu milioni 1.8 wako Zanzibar.

Kwa upande wa wanawake ni milioni 31.6 sawa na asilimia 51 wakati wanaume ni milioni 30 sawa na asilimia 49.

“Ninapenda kuwatanzangia Tanzania ina idadi ya watu milioni 61.74. kati yao wanawake ni milioni 31.6 sawa na asilimia 51 na wanaume milioni 30.05 sawa na asilimia 49 ya watu wote,” amesema.

Rais Samia amesema Mkoa wa Dar es Salaam ndio unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu nchini ambao ni milioni 5.3 sawa na asilimia saba na kufuatiwa na Mwanza watu milioni 3.6 sawa na asilimia sita.

Rais Samia katika kipindi cha miaka 10 kuna ongezeko la watu milioni 16.8 sawa na asilimia 3.2.

“Miaka kumi iliyopita Tanzania ilikuwa na watu 44, 928, 923 hii inaonyesha kumekuwapi na ongezeko la watu milioni 16,812,197 sawa na ongezeko la asilimia 3.2 ya waliokuwepo kati ya mwaka 2012 na mwaka 2022.

“Tanzania Zanzibar, Idadi ya watu imeongezeka kutoka 1,303,569 mwaka 2012 hadi watu 1, 889,773 mwaka 2022 sawa na ongezeko la asilimia 3.7” amesema.




from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/g5wZsiX
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story