Yanga yatumia mbinu za Simba, Ibenge alia na Mayele




KATIKA kuhakikisha Yanga wanapata matokeo mazuri mechi ya marudiano dhidi ya Al Hilal ya Sudani, mabosi wa Yanga wameanza kutegua mitego ya wapinzani wao nchini humo na wataanza na staili ya Simba iliyofanya Angola. Mwanaspoti linajua kwamba Kocha Nabi Mohammed ana mtandao mkubwa nchini Sudani na yuko kazi kwa sasa.

Yanga itakuwa na kibarua cha kupambana kufuzu hatua ya makundi baada ya mechi ya awali iliyochezwa Uwanja wa Mkapa kupata sare ya 1-1. Yanga wanahitaji sare ya mabao 2-2 au ushindi ili kufuzu makundi.

Taarifa ambazo Mwanaspoti imezipata ni kwamba mabosi wa timu hiyo wameandaa kila kitu kwa ajili ya safari ikiwemo kupima Uviko-19 na majibu yao watayapata siku ya Ijumaa saa chache kabla ya safari.

Awali walipanga kuondoka kesho Alhamisi lakini viongozi wameona ni bora wachelewe kwenda Sudani ili watumie majibu ya Uviko-19 kutoka nchini ambayo yatawafanya waingie nchini humo vizuri na kutoka siku hiyohiyo baada ya mechi.


Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga ni kwamba wataondoka Jumamosi alfajiri na watafika Sudani asubuhi kisha jioni watafanya mazoezi kwa ajili ya mchezo wa Jumapili. Mbinu hiyo waliitumia Simba walipokwenda kuichapa Agosto Jijini Luanda.

“Majibu ya vipimo vyetu yanakuwa hai kwa saa 72, hivyo tutaingia Sudani na kutoka bila kizuizi, hatujataka kuwahi halafu tufanyiwe vipimo vya Uviko-19 kule kwani lolote linaweza kutokea, baada ya mechi tutarudi nyumbani,” alidokeza mmoja wa viongozi wa Yanga.

Rais wa Yanga, Hersi Said alisema kuwa; “Tumepata msaada mkubwa kutoka kwa balozi wetu kule Khartoum (Sudan), mashindano ya Afrika yamekuwa na mazingira magumu hasa ya ugenini.”


“Tumepunguza idadi ya siku za kukaa ili kupunguza hizo hujuma, tupo makini katika hii mechi, tuna wachezaji wazoefu ambao wanajua mazingira ya ugenini na kilichotokea Dar es Salaam ni sehemu ya matokeo ya mpira na tulijitengenezea nafasi nyingi,” alisema Hersi.

Mshambuliaji wa zamani Yanga, Herry Morris alisema viongozi wa Yanga wanafanya jambo zuri kwani timu wanayoenda kukutana nayo siku zote inapokuwa nyumbani mechi zake lazima ziwe na malalamiko.

“Yanga wanaijua vizuri Al Hilal kwahiyo kuchelewa kwao ni katika upande wa faida wakitafuta matokeo, hujuma ni nyingi sana lakini wakiziepuka zote kama wanavyofanya sina shaka na matokeo ya ndani ya uwanja,”alisema Morris.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Zamoyoni Mogela ambaye alisema; “Kule kuna siasa nyingi kwahiyo sioni kama kuna ubaya sana wakiwa watafuta matokeo.” Yanga imepania kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo msimu huu.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/ysfBqun
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI