Familia Wafunguka Kuhusu Picha Aliyopost Profesor Jay "Ilipostiwa Kwa Bahati Mbaya"


Saa chache zilizopita kwenye ukurasa wa Instagram wa Mkongwe wa Bongofleva Profesa Jay @professorjaytz upande wa Insta story kulipostiwa picha yake akionekana na Mke wake wakihojiwa kwenye red carpet, kitendo kilichoamsha furaha ya Mashabiki wengi kuona Mkali huyo ameimarika kiafya na wengine kuamini ameanza kuhudhuria matukio mbalimbali.

Msemaji wa Familia ya Haule @blackchatta aliyepatikana kuzungumzia hilo ameiambia AyoTV kuwa ni kweli post hiyo (ipo kwenye swipe) ilichapishwa na Profesa Jay mwenyewe lakini kwa bahati mbaya kwa sababu anatumia simu zake zote kwa sasa na huwa anaingia kwenye mitandao kuperuzi japo hajawahi kupost chochote toka January 23 2022.

“Anatumia simu zake zote sasa hivi na anaingia kwenye social media, anasoma anaona matukio yote lakini mambo ya kupost haya kwa sasa bado, anaruhusiwa kutumia simu kuangalia vitu, ile ni picha ya siku nyingi alipost kwa bahati mbaya iliteleza kwenye mikono yake lakini yuko fresh tunamshukuru Mungu”

“Watu wasiwe na hofu kama tuliyokuwa nayo mwanzo sasa hivi yupo nyumbani anaendelea na mazoezi” ——— amemalizia @blackchatta


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/RvlX1Cb
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI