Hatimaye Talaka ya Kanye West na Kim Kardashian Yakamilika


Hatimaye mastaa Kanye West (YE) na Kim Kardashian mchakato wao wa Talaka umekamilika Jumatatu hii, wameripotiwa na TMZ kufikia maridhiano ya Talaka huku Kanye West atatakiwa kumlipa Kim Kardashian kiasi cha $200k ambazo ni zaidi ya TZS Milioni 466 kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya watoto wao.

Lingine lilioangaziwa kwenye maridhiano hayo ni haki sawa katika malezi ya watoto wao. Tovuti ya TMZ imeeleza. Na iwapo mmoja wao atashindwa kushiriki vyema, mwingine anapewa nafasi ya kufanya uamuzi kwa chaguo la msingi.

Itakumbukwa, Mwanamama Kim Kardashian mwezi Februari, mwaka jana alifungua shauri mahakamani la kudai Talaka baada ya kuwa kwenye ndoa kwa takribani miaka 7 na Kanye West.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/iWybTa1
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI