Mwigizaji Ray Kigosi Afunguka Kauli ya Kubebwa na Kanumba "Mimi Ndio Nilimtoa Kanumba"


Muigizaji mkongwe kutokea kwenye kiwanda cha Bongo Movie, @raythegreatest hii leo Nov 25 ameongea na waandishi wa habari kwaajili ya kutangaza dili lake na kampuni ya ulinzi nchini #k4ssecurity kama balozi mpya wa kampuni hiyo. Mbali na Jambo hilo ambalo ndilo lililokuwa lengo hasa la press conference yake, Ray amedokeza ujio wa kazi zake mpya na kubwa, lakini pia ametaja sababu kubwa ya kudumaa kwa tasnia ya uigizaji nchini, ni kutokuzalishwa kwa waigizaji wapya wenye vipaji vya kufikia levo za kina Wema Sepetu.

Ray amedai anarudi kwenye sanaa kuiboresha upya kwa kuleta vipaji vipya kwasababu ana karama hiyo ya kuibua talents kali, Pia amedai anashangaa watu wakisema alikuwa anabebwa na Kanumba, wakati haipo hivyo sababu Kanumba alitokea kwenye mikono ya Ray, waigizaji kama Uwoya, Wolper, Johari na wengine kibao wakubwa kama Thea walitokea kwenye mikono yake.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Pm6hwCJ
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI