Polisi Watatu Wauawa Kwenye Msafara, Kiongozi Atekwa



Kundi la watu wenye silaha wamewaua Polisi watatu waliokuwa wakisindikiza msafara na kisha kumteka Meneja wa kampuni ya mafuta ya IGPES Group of Oil and Gas, Seni Awosika aliyekuwa na kiasi kikubwa cha pesa na kisha kutokomea kusikojulikana.


Maafisa wa upelelezi wa Kamandi ya Polisi ya Rivers wamesema wameanza msako wa kuwatafuta watu hao ambao walifanya tukio hilo kwenye barabara ya juu ya Rumuokoro iliyopo eneo la Port Harcourt, ambao ni mji mkuu wa jimbo hilo majira ya saa tatu usiku wa Novemba 24, 2022.


Eneo la tukio juu ya Daraja la Rumuokoro lililopo jimbo la River Port Harcourt, Nigeria. Picha ya Within Nigeria.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema, watu hao wenye silaha waliufuata msafara huo ambapo walifanikiwa kuunasua na kuwapiga risasi Polisi hao kabla ya kumteka nyara Meneja huyo na walikuwa wamevalia sare za kijeshi.


Kwa mujibu wa Msemaji wa Polisi wa eneo hilo, Grace Iringe-Koko amesema, “Polisi watatu waliokuwa wakimsindikiza mtendaji huyo waliuawa huku mwanamume huyo akitekwa nyara na kupelekwa eneo lisilojulikana na walijifanya wapo doria ya kijeshi katika gari la kijani kibichi, wakiashiria msafara huo kusimama kabla ya kufyatua risasi na kuwaua polisi.”


Serikali yakataa mazungumzo ya amani


Polisi wa Doria nchini Nigeria. Picha ya Nigerian news direct.

Nyerere na Tambo ndani ya ofisi ya ukombozi

Hata hivyo, inaarifiwa kuwa utekaji nyara kwa ajili ya fidia ni jambo la kawaida katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika, na Wahalifu wamekuwa wakilenga wafanyabiashara matajiri na wakulima maskini, ambao ni wahasiriwa wa utekaji nyara mkubwa kaskazini mwa nchi.


Delta ya Niger, ni mji wa rasilimali ya mafuta na gesi yenye thamani ya mabilioni ya dola ambao wakazi wake wanaishi katika hali ya umaskini kutokana na miongo kadhaa ya uchafuzi wa mazingira na hivyo kutelekezwa, huku vitendo vya rushwa na ukosefu wa haki ukiwa wa kiwango cha juu.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/QiAtCqU
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI