Serikali yatangaza Rasmi vita na Al-Shabaab

 


Vita kamili dhidi ya wanamgambo wa Al-Shabaab imetangazwa rasmi, na kuidhinishwa kwa juhudi za kupambana na ugaidi ambazo licha ya ya mafanikio yake ya kijeshi ya siku za mwanzo huenda ikawa vigumu na vikadumu kwa muda mrefu kutokana na uhalisia.


Vita hiyo imetangazwa na Serikali ya Somalia, kulikabili kundi hilo lenye mafungamano na al-Qaeda lililofukuzwa kwenye miji mikubwa muongo mmoja uliopita lakini bado linashikilia maeneo mengi ya mashambani ambako makundi ya wanamgambo yameungana kwa ajili ya mapambano.

Aidha, inaarifiwa kuwa koo mbili za nchini humo ambazo zimechoshwa na utawala wa Al-Shabaab, zilianzisha uasi dhidi ya kundi hilo uliosambaa haraka katika mikoa ya Hirshabelle na Galmudug na mwezi Septemba ulipata usaidizi wa makomandoo waliopewa mafunzo na Marekani.


Kwa upande wake, Mtafiti kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Migogoro (ICG0, Omar Mahmood amesema nia ya Serikali ni kuendeleza kasi ya sasa na kuondoa uasi kama huo katika maeneo yote yanayoshikiliwa na Al-Shabaab nchini Somalia.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/vbEkgY9
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI