Zitto Kabwe: Hatujafunga ndoa na CCM



KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameeleza kuwa chama hicho ni tofauti na Chama Cha Mapinduzi (CCM), pamoja na vyama vingine vya siasa vya upinzani. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mwanasiasa huyo ametoa kauli hiyo katika mahojiano yake na Kituo cha Televisheni cha ITV, yaliyorushwa mubashara jana Jumatatu kuhusu madai ya ACT-Wazalendo kuwa mshirika wa CCM.

“Kwenye siasa kuna mitizamo tofauti na ni wajibu wa chama kuhakikisha kinasimamia yale malengo ambayo kinataka kuyafikia, sisi ni tofauti na CCM, Chadema, CUF na vyama vingine vyote. Tunafanya siasa zetu kwa mujibu wa maamuzi yetu. Kama kuna mtu ambaye anatutazama kwa hivi unavyosema ni mtizamo wake na sisi ni wajibu wetu kumuonyesha hapana sisi tuko tofauti,” alisema Zitto.

Katika hatua nyingine, Zitto alisema ACT-Wazalendo hakina mgogoro na chama chochote cha siasa nchini, na kwamba wanachama na viongozi wake wanajibu hoja za wanachama wa chama kingine, pale ambapo shabaha na malengo ya chama chao yanapoingiliwa.


“Kama utaona kuna mahala ambako wanachama wetu wanajibizana na wanachama au viongozi wa chama kingine, ni pale ambapo tumechokozwa au tunaingiliwa kwenye shabaha na malengoi yetu. Lazima tuheshimu kwamba kuna njia tofauti za kufanya siasa na tukiheshimiana naamini hawataona ugomvi na majibizano yanayotokea. Tatizo linatokea pale ambapo mtu mmoja anavyotaka wengine wamfuate, hiyo siyo demokrasia,” alisema Zitto.

Alipoulizwa kwamba ACT-Wazalendo kinatofautiana vipi na vyama vingine vya siasa, Zitto alijibu “jambo kubwa ninaloliona ni tofauti na vyama vingine na inanifanya nishawishi watu wengine wajiunge kwenye chama ambacho kinabeba matumaini ya Watanzania, ni uwezo wetu wa kuangalia mbele na kutoka kwenye siasa za kulalamika kwenda kwenye siasa za kuibua masuala na mapendekezo ya kuyatatua.”

Aidha, Zitto amesema chama chake kinaendelea kukua kwa kasi, huku akijigamba kuwa kina nguvu Tanzania Bara na Zanzibar.


“Tuna chama ambacho kinakua kwa kasi, kinapata wanachama wengi, kinaimarika kitaasisi, ni chama ambacho kina nguvu pande zote mbili katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, upande wa Tanganyika na Zanzibar. Chama ambacho kina viongozi mahiri ambao wamesambaa pande zote,” alisema Zitto.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/wSb9Jht
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story