Azam Wafunguka "Hatuna Mpango Wowote na Fei Toto"


Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC Abdulkareem Amin ‘Popat’ amesema klabu yao haina mpango wowote wa kumsajili Kiungo wa Yanga Feisal ‘Fei Toto’. Popat amekanusha taarifa za kuwaniwa kwa Kiungo huyo alipohojiwa na Kituo cha Radio cha Wasafi FM mapema leo Alhamisi.

Amesema hata wao wanaona na kusikia Klabu yao inatajwa kwenye sakata la Mchezaji huyo, lakini hawana mpango wowote wa kumsajili.

“Sisi wenyewe tunasoma tu mitandaoni kuhusu Feisal Salum. Hakuna siku tuliyowahi kukaa na kusema tunamtaka Feisal. Yule ni mchezaji mzuri na tegemeo katika timu yake ya Yanga na timu ya taifa.” - Popat.

“Hakuna timu ambayo haiwezi kumtamani Feisal, lakini sisi kama Azam FC hatuna taarifa ya namna hii maana hakuna sehemu tuliyosema wala kuandika kuwa tunamtaka Feisal.“ - Popat.

Fei Toto amekua gumzo kwa sasa katika vyombo vya Habari pamoja na mitandaoni, kufuatia taarifa aliyoiweka katika Ukurasa wake wa Instagram mwishoni mwa juma lililopita, akiwaaga Mashabiki, Wanachama na Wachezaji wenzake wa Yanga na baadae Uongozi kumjibu.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/mFCXU2Q
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI