Ismail Rage aingilia kati sakata la Fei Toto



Mwenyekiti wa zamani wa Simba SC Ismail Aden Rage amewataka viongozi wa klabu za Young Africans na Azam FC kutua busara kumaliza sakata la Kiungo Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’.

Siku chache zilizopita kumekuwa na mvutano mkubwa kutokanana Azam FC kuhusishwa kumrubuni mchezaji huyo wa Young Africans kuvunja mkataba ili ajiunge na Timu hiyo.

Rage amesema haoni sababu kwa viongozi wa pande hizo kulimbana ukizingatia kanuni zote zipo wazi hivyo ni vyema kila upande ukakubali kukutana kwa pamoja na kumaliza jambo hilo.

“Itapendeza kama viongozi wa timu hizi mbili wakatanguliza busara mbele na sio malumbano na chuki ambazo hazina afya kwenye mpira wetu, ingawa matukio kama haya yanaonesha mpira wa Tanzania sasa unakuwa, kitu cha msingi viongozi wangekutana na kuzungumza”

“Ukiangalia kisheria upo upande una makosa lakini kabla hatujafika huko ni vyema hekima na busara ikatumika ili tuendelee kukuza mpira wetu na kutawaliwa na jazba na chuki mwenyewe kwa wenyewe.” amesema Rage

Feisal Salum ‘Fei Toto’ kwa sasa yupo nyumbani kwao Zanzibar na jana Alhamis alionekana akichezea Klabu yake ya zamani JKU katika mchezo wa Kirafiki dhidi ya Mlandege.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/OuJY2y0
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI