Mjukuu wa Bob Marley, Joseph ‘Jo’ Mersa Marley Afariki Dunia



Kwa mujibu wa TMZ ambao ni miongoni mwa vyombo vya kwanza kutoa taarifa ya kifo hicho, Joseph, maarufu Jo Mersa, alifariki Jumanne Desemba 27, 2022 kutokana na matatizo yanayohusiana na pumu, ingawa maelezo ya kina kuhusu kifo chake bado hayajawekwa wazi.


Joseph, ambaye ni mtoto Stephen Marley, muda mchache uliopita alijiunga na chuo cha Miami Dade na kusoma uhandisi wa sauti (audio engineering) baada ya kukaa miaka yake kadhaa huko Jamaika.



Mwaka 2014 aliachia Ep yake iliyoitwa “Comfortable”, ambayo ilikuwa na nyimbo kama vile “Rock and Swing” na “Bogus.” Pia alitoa wimbo uliovuma sana, “Burn It Down,” mwaka wa 2016 na mwaka jana alifanikiwa kualiachia Ep yake ya 2, “Eternal,”.





from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/CQUTWMc
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI