Vibaka nchini Ghana wamliza rapa Meek Mill

 


Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 35 kwa sasa yuko nchini Ghana ambako alihudhuria kwaajili ya kutumbuiza katika Tamasha la Muziki la Afro Nation 2022.


Meek Mill alionekana kujiburudisha katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, baada ya kuenea kwa video clips mitandaoni akionekana rapa huyo nyota kutoka nchini Marekani akiendesha piki piki na vijana kadhaa wa mitaani.


Hata hivyo, saa chache kabla ya onyesho lake katika tamasha la Afro Nation, alibaini na kuweka wazi kuwa vibaka wlimchomolea simu yake ya mkononi bila kujua huku akieleza kuwa anahisi ni katika kipindi ambacho walikuwa wakikatiza mitaa mbali mbali ya nchini ya Ghana.


Katika chapisho kwenye kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram (Insta story) Meek Mill alitoa wito kwa yeyote aliyechukua simu yake airejeshe haraka.


“Ni kama waliingiza mikono mfukoni mwangu nakupora simu, tafadhali nirejeshee ikiwa utaipata” ameandika Meek mill.


Licha ya uchungu wa kupoteza simu yake, Inaelezwa kuwa Meek Mill hakusita kuporomosha burudani ya kiwango cha juu, iliyowasisimua mashabiki wake kwenye tamasha la Afro Nation, ambalo lilifanyika Accra Marine Drive, Black Star Square.


Nyota huyo alitumbuiza baadhi ya nyimbo zake zilizovuma sana, huku umati wa watu uliokuwa umejaa wakiimba naye pamoja muda wote ambao rapa huyo alikuwa jukwaani akitumbuiza.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/kva0tYM
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI