Vichwa vya Vilivyovunja Pambano la Pialali, Mfaume
Pambano la usiku wa mabingwa kati ya mabondia Idd Pialali na Mfaume Mfaume limeshindwa kumalizika kwa kupatikana mshindi kutokana madai mabondia hao kupigana vichwa kwa mujibu wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBRC.
Pambano hilo ambalo lilikuwa la raundi kumi katika uzani wa Super Walter ambalo limechezwa kwa raundi moja kabla ya vunjika kutoka na mabondia hao kugongana vichwa vilivyopelekea Pialali kupasuka usoni.
Katika pambano hilo ambalo limepigwa juzi Jumatatu kwenye Ukumbi wa AICC Arusha, Lake Nyasa halikuweza kuendelea kutokana na tukio hilo huku promota akipewa nafasi ya kulirudia tena pambano hilo kwa kuwa halikuweza kupatikana mshindi.
Katibu mkuu wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini, TPBRC, Yahaya Poli akiwa na rais wa kamisheni hiyo, Chaulembo Palasa alitangaza kuwa pambano hilo halina mshindi baada ya kujiridhisha wazi kuwa mabondia hao wote waligonga vichwa na kuamua kuvunja pambano hilo.
Lakini kwa upande wa Pialali alisema kuwa tukio lilotokea katika pambano hilo halikuwa matarajio yake huku akisisitiza atakuwa tayari kwa ajili ya pambano la marudiano.
Mfaume yeye alisema kuwa matokeo yaliotokea siyo jambo alilolitarajia kwa kuwa tayari viongozi walishalitolea maelezo hivyo hatoweza kuliongelea zaidi ya kuangalia mabondia wa nje katika mapambano yake ya jayo.
Mabondia wengine walifanikiwa kushinda katika pambano hilo la Usiku wa Mabingwa ni Karim Mandonga aliyemchapa Alibaba Tarimo wakati Hassan Ndonga akimchapa kwa KO ya raundi ya kwanza Yamikani Mkandawire.
Shabani Ndaro wa Arusha amefanikiwa kumaliza utawala wa Shaban Kaoneka kwa pointi wakati Halima Vunjabei akimtwanga kwa TKO, Yohana amefanikiwa kumchapa Yamikani Mkandawire kutoka Malawi,Osama Allabi akimchapa Salim Omary kwa pointi, Hamad.
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/0R4u8Lz
via IFTTT
Comments
Post a Comment