Big Six Yaanza Kusambaratika Vipande Vipande Kabla ya Kufikia Malengo yao

Big Six Yaanza Kusambaratika Vipande Vipande Kabla ya Kufikia Malengo yao

Kinacho endelea hivi sasa ni ugomvi wa kutupiana vijembe kati ya #wolper na #auntyezekiel ambao ni miongoni mwa waigizaji wa kike nchini wanaounda Big 6, wengine wakiwa Irene Uwoya, Wema Sepetu, Elizabeth Michael (Lulu) pamoja na Frida Kajala.


Moja ya malengo ambayo walijiwekea na kuahidi kwa mashabiki wao, ni kuja na projects za pamoja, yani watarudi na filamu zao wenyewe wakiwa ndani na kufanya ishu nyingine zitazo wahusisha wao wenyewe, hii ilikuwa ni mwaka 2022. Mwanzoni ilikuwa ni ugomvi wa Wema Sepetu na Lulu ambao ulisuluhishwa na Martin Kadinda pamoja na members wengine wa Big 6.


Hasa imekuwa tofauti kwa sasa ambapo Aunty Ezekiel na Wolper wameingia kwenye ugomvi mzito, ikiwemo kila mmoja kum-unfollow mwenzie, lakini pia kila mmoja kuwa na ukaribu na Ex wa mume wa mwenzie, yani Wolper kuwa upande wa Ruby na Aunty kuwa Upande wa Mwanamke aliyezaa na Rich Mitindo. Wajuzi wa mambo wanadai, Wolper yupo kwenye harakati za kupunguza waaalikwa wote ambao ni marafiki zake wa karibu ila hawakutokea kwenye harusi yake.


Malengo makubwa yalikuwa ni ufanyaji kazi wa pamoja, ukizingatia ndio waliokuwa habari ya mjini enzi za Bongo Movie ikiitwa Bongo Movie, hivyo walitaka kuwarudisha mashabiki zao enzi hizo. Ni ngumu kuliona hili likitokea baada ya haya yanayoendelea.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/bVvCk6W
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI