Mwijaku Aguswa na Diamond Platnumz Kutotokea Kwenye Event ya Marioo

Mwijaku Aguswa na Diamond Platnumz Kutotokea Kwenye Event ya Marioo

Mwijaku wewe umesoma mambo ya Biashara nadhani unaelewa. Hivi sasa Diamond Platnumz sio mtu wa kutokea hovyo kwenye Events za watu, tena zilizoandaliwa na Wapinzani wake kibiashara na wenye bifu la kiukweli ukweli, tangu lini Majizzo na Diamond zikaiva? EFM na TVE wamekaa muda gani hawapigi nyimbo za Diamond then leo hii aende kutafuta nini? Kwanza Diamond angetokea hapo ange-promote Bure album ya Marioo, Mpaka sasa kuna watu hawajui kama Jana Marioo alikuwa na tukio ila Diamond angetokea kila mtu angejua kwamba Marioo ana tukio.

Diamond alitokea kwa Barnaba na Jux kwa sababu waliingia Partnership. Hivi sasa Diamond hawezi kumsindikiza mtu kwenye utajiri. Ataku-support kama na yeye pia anaingiza kitu. Kama Wasafi TV na FM ndio ingekuwa Inasimamia Uzinduzi wa hiyo Album basi angetokea.

@mwijaku kumbuka HARMONIZE hajatokea, kwanini yeye humlaumu?

Ipo hivi, Marioo kwenda kwenye events za Diamond ni lazima na ni Muhimu, aende akajifunze mkubwa wake anafanya nini, ila Diamond kwenda kwa Marioo ni uamuzi tu.

Pia tambua kwamba Wasanii wa WCB ni Brands huwa hawatokei hovyo hovyo, ndio maana hujaona Mbosso, Zuchu, Lava Lava na Darlin.

Lakini Diamond hajamtupa jumla Marioo ametuma Wawakilishi, Sallam Sk na Wengine Kibao wametokea.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/2vWGE30
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI