Mwili wa Nemes Tarimo Aliyefariki Vitani Ukraine Waagwa Bila Kufungua Jeneza


Mwili wa Mtanzania Nemes Tarimo ambaye alifariki October 24,2022 akiwa vitani nchini Ukraine baada ya kujiunga na Jeshi binafsi la Urusi la Wagner Group tayari umeagwa nyumbani kwa Familia Mbezi Dar es salaam baada ya kupokewa katika Uwanja wa Ndege wa J.K Nyerere Dar es salaam leo January 27,2023 ambapo unatarajia kusafirishwa leo hadi Mbeya kwa maziko.

Familia imesema kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao jeneza halitofunguliwa hivyo Ndugu, Jamaa na Marafiki wameaga picha na jeneza ““Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu tutatumia mtindo wa kuaga sanduku pamoja na picha hatutaweza kulifungua sanduku kwasababu zilizo nje ya uwezo wetu”

Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali ya Tanzania iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki mapema Wiki hii, Nemes alifariki akiwa vitani nchini Ukraine baada ya kujiunga na Jeshi binafsi la Urusi la Wagner Group akiwa anatumikia sehemu ya kifungo chake cha miaka saba alichofungwa kwa makosa ya kihalifu.

Waziri Tax alinukuliwa akisema “Tarimo akiwa gerezani alipewa nafasi ya kujiunga na kikundi cha kijeshi cha Wagner kwa ahadi ya kulipwa fedha lakini kwa ahadi ya kuachiwa huru mara baada ya vita na umauti ulimkuta October 24,2022 na Wizara ikawasiliana na Serikali ya Urusi ili kukabidhiwa mwili”

“Nemes Tarimo alikwenda nchini Urusi mwaka 2020 kwa masomo ya shahada ya uzamili katika fani ya biashara , March 2022 alihukumiwa kifungo cha miaka saba kwa vitendo vya uhalifu”


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/upPWD4I
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI