Sky Tanzania Ausifia Uzinduzi Album ya Marioo "Umefana Sana Sijawahi Kuona"


Uzinduzi wa #TKYK ya @marioo_tz umefana sana. Kuna namna nyimbo zake zinasound vizuri mno zikipigwa live. Huenda hii imechangiwa na bendi aliyokuwa nayo, sound nzuri (shout outs kwa @majizzo), na pia namna Dj alivyosynch na bendi.

Imagine ngoma kama Mi Amor imesound vizuri kuliko original, wale back vocalists walikuwa on point kiasi cha kuhisi upo kwenye gospel concert ( I mean muziki ulikuwa mwingi na powerful sana).

Amini kwamba!

Ni wazi kuwa Marioo alifanya rehearsal heavy kupata ubora huu kwa namna pia yeye na dancers walivyokuwa organised jukwaani.

Ukamilifu wa shughuli hii hauwezi kuongelewa bila mchango mkubwa wa wasanii waliompa support. @juma_jux alivyoimba naye na kumpa maua yake ikiwemo kumtambua Marioo kama mwandishi wa hit yake Unaniweza na walivyoperform Nice (Kiss) jukwaani.

Tiktoker wa Kenya @moyadavid1 ambaye mchango katika wimbo Mi Amor unaeleweka, alipanda kwa surprise na kucheza style yake maarufu na kumpa Marioo maua.

Then, kwa mbali sauti tamu ya kike ikawa inasikika, kidogo nihisi Jovial anapanda, surprise ikawa ni @officialnandy ambaye oh my, she killed it 🙌🙌

Ikaja zamu ya @officialalikiba kuungana na Marioo jukwaani. Hapa ukumbi ulilipuka kwa shangwe. I Miss You ni wimbo wenye melody tamu sana, so imagine kwa ubora wa bendi ya jana unapata nini? Perfection!

Kisha Kiba akamalizia na Utu! Hapa akathibitisha ufalme wake. Kirahisi tu unamuona anaimba ila vocals ni balaa!

@rayvanny came through! Kwa pamoja wakatumbuiza collabo yao. Ila nilimnyooshea pale alipopiga freestyle na kuweka utani uliovunja mbavu watu. Very creative!

Kumalizia. Ilipendeza kuona mastaa wengi sana wamejitokeza kwenye event hii.

It's was a success!


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/IlzRAjC
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI