Waarabu Watuma Mashushushu Yanga Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika





KOCHA Mkuu wa Klabu ya US Monastir ya Tunisia, Darkov Novic ameweka wazi kuwa wanatambua wapinzani wao Yanga ni miongoni mwa timu bora katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika lakini mipango yao ni kuhakikisha wanapata ushindi mkubwa kwa kuwa wanawajua vizuri na wamekuwa wakiwafuatilia wanapocheza.

Novic ametoa kauli hiyo kuelekea katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Yanga inayonolewa na Kocha Nasreddine Nabi raia wa Tunisia katika  unaotarajia kupigwa Februari 12, mwaka huu nchini Tunisia.

Yanga ambao inaenda kwenye mchezo huo ikiwa inaongoza ligi kwa pointi 56 wakati wapinzani wao hao wakiwa katika michuano hiyo wakiwa katika nafasi ya kwanza katika kundi B wakiwa na pointi 22 kwenye ligi kuu ya nchini humo.

Yanga kwa asilimia kubwa ilikuwa ikitegemea mabao ya Fiston Mayele na sasa wamemuongeza straika mwingine Kennedy Musonda aliyejiunga nao kwenye dirisha dogo lililofungwa Januari 15, mwaka huu.



Hivyo Novic na wapambe wake watakuwa na kazi ya kumsoma Musonda atakapokuwa akicheza mechi za Dar kuanzia keshokutwa Jumapili dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Novic alisema kuwa, wanajua ukubwa wa wapinzani wao lakini wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata matokeo ya ushindi katika mchezo wa kwanza katika kundi lao ili kuweza kupata mwanga mzuri wa kwenda kwenye hatua inayofuata.

“Tunataka kuona tunapata matokeo kwa sababu hatua ambayo tupo kwa sasa siyo nyepesi maana kila timu imekuwa ikijiandaa kuona inaweza kuongoza kundi na kitu kizuri tunaenda kuanzia nyumbani, kwetu inatupa nafasi kubwa ya kufanya mambo makubwa.


“Kuhusu wapinzani wote tunawajua vizuri na tumejiandaa kwenda kucheza kwenye mazingira ya aina yoyote kutokana na ukubwa wa michuano yenyewe, tumewaona wakicheza hapa na Club Africain lakini bado tumekuwa tukiwafuatilia kwa kuhakikisha tunaweza kupata matokeo,” alisema Novic.

Ikumbukwe, Yanga imepangwa Kundi D sambamba na Monastir ya Tunisia, Real Bamako ya Mali na TP Mazembe ya DR Congo.

Stori na Ibrahim Mussa



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/fO8dRl7
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI