Kocha Wa Yanga Aiteka Shoo Leo Jumapili Dhidi Ya Real Bamako Ya Mali

Kocha Wa Yanga Aiteka Shoo Leo Jumapili Dhidi Ya Real Bamako Ya Mali


KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, ameiteka shoo yote katika mchezo wa leo Jumapili dhidi ya Real Bamako ya Mali, baada ya kutambulisha mbinu mbili kali za ushindi wakiwa ugenini.


Yanga ambayo inashika nafasi ya pili kwenye Kundi D la Kombe la Shirikisho Afrika, leo Jumapili itapambana na Real Bamako, mchezo ukipigwa Stade du 26 Mars, dimba lililopo Kusini mwa Mji wa Bamako nchini Mali.


Katika mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, Yanga imepania kuibuka na ushindi ili kuweka mazingira mazuri zaidi ya kufuzu robo fainali ya michuano hiyo.


Juzi Ijumaa katika mazoezi yao ya kwanza yaliyofanyika kwenye kituo cha Stade Malien, Yanga ilionekana kufanyia kazi zaidi mazoezi ya kufunga kutumia mipira ya krosi.


Mbali na zoezi hilo, pia benchi la ufundi la timu hiyo lilitoa program ya kufunga mabao kwa mashuti makali nje ya eneo la hatari la wapinzani.


Katika mazoezi ya kufunga kwa kutumia krosi, program hiyo iliwataka mabeki wa pembeni kupiga krosi hizo ambao ni Djuma Shaban anayecheza beki wa kulia na beki wa kushoto, Joyce Lomalisa.


Fiston Mayele na Stephane Aziz Ki, walionekana kuwa na uchu mkubwa wa kufunga mabao katika mazoezi hayo yaliyosimamiwa na Kocha Msaidizi, Cedric Kaze kwani kila mmoja alifunga kutumia krosi zilizopigwa na mashuti ya mbali.


Ikumbukwe kuwa, Yanga katika mchezo uliopita dhidi ya TP Mazembe ambao ilishinda mabao 3-1 nyumbani, kati ya mabao hayo, moja pekee lilitokana na krosi ya pembeni.


Bao hilo ni lile la kwanza lililofungwa na Kennedy Musonda dakika ya 7 ambaye aliunganisha faulo iliyopigwa na Djuma Shaban kutokea upande wa kulia.


Mabao mengine mawili yaliyofungwa na Mudathir Yahya (dk 11) na Tuisila Kisinda (dk 90+2), yalitokana na mashambulizi ya kushtukiza.


STORI: MWANDISHI WETU, BAMAKO



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/60Bjk3p
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI