Yanga Wakomaa Na Hesabu Za Robo Afrika Uwanja Wa Mkapa Dar

 


UONGOZI wa Yanga umetamba kuwa bila kujali matokeo yao ya mchezo wa jana Jumapili dhidi ya Real Bamako, kikosi chao kina nafasi kubwa ya kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kushinda michezo yao miwili ya nyumbani dhidi ya Real Bamako ya Mali na US Monastir ya Tunisia.


Yanga jana Jumapili walishuka kwenye Uwanja wa Machi 26, nchini Mali kuvaana na Real Bamako ya Mali katika mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.


Mara baada ya ushindi dhidi ya TP Mazembe, Yanga sasa imebakiwa na michezo miwili ya nyumbani dhidi ya Real Bamako na US Monastir.


Akizungumzia malengo yao katika mashindano hayo Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema: “Leo (jana), Jumapili tunatarajiwa kuwa na mchezo dhidi ya Real Bamako ambao ni muhimu kwetu kupata matokeo ya ushindi au angalau sare kwa ajili ya kuweka sawa hesabu za kucheza robo fainali ya mashindano haya.


“Lakini hata kabla ya mchezo huu na bila kujali matokeo yake tayari tuliweka wazi kuwa nguvu kubwa tumewekeza katika pointi tisa za Uwanja wa Benjamin Mkapa yaani kuhakikisha tunashinda mechi zetu tatu za nyumbani, tayari tumeshinda na TP Mazembe bado sita ambazo tunazitaka kwa hali yoyote.”


Stori: Joel Thomas



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/E6J2zwN
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story