Droo robo fainali ligi ya mabingwa, Shirikisho Jumatano ijayo





 
Droo ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika na kombe la Shirikisho, itafanyika Jumatano ijayo April 05 huko Cairo, Misri


Wananchi Yanga watakuwa miongoni mwa timu nane ambazo zitahusika katika droo ya robo fainali ya kombe la Shirikisho

Mechi za kuhitimisha makundi zinapigwa mwishoni mwa wiki hii Yanga ikitarajiwa kuondoka Dar leo kuifuata TP Mazembe kwa ajili ya mchezo utakaopigwa April 02 huko Lubumbashi pia Simba ni miongoni mwa timu nane zilizofuzu robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa ikimaliza kwenye nafasi ya pili kutoka kundi C

Mechi za kuhitimisha makundi zinapigwa mwishoni mwa wiki hii Simba ikimaliza mechi yake ya mwisho dhidi ya Raja Casablanca huko Morocco mchezo ukipigwa saa saba usiku wa kuamkia Jumamosi

Yanga imepania kumaliza kileleni mwa kundi D ili kuanzia mechi ya robo fainali ugenini na kisha kumalizia nyumbani huku

Simba ikiwa tayari kukutana na yeyote katika hatua ya robo fainali kwani hakuna timu nyepesi katika hatua hiyo




from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/VGM7rCo
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI