Gigy Money "Nimeongea na Mo J , Nimemsamehe na Ninampenda"


Kilichotokea wiki hii kwa Gigy Money na Baba mtoto wake kimeuza magazeti na kutawala kwenye mitandao ya Kijamii vile vile kubaki gumzo vinywani mwa watu. Gigy Money ameamua kusafisha hali ya hewa kwa andiko lake hapa instagram masaa machache yaliyopita kuhusiana na tukio lile la mzazi mwenzake kumfuata akiwa na polisi.

Kwenye andiko lake Gigy amefunguka kwamba, amezungumza na Mo J na amemsamehe kwa alichokifanya. Lakini pia kwa ustawi wa mtoto wao (Mayra) Gigy amefungua moyo na kusema sasa ameondoa kinyongo na kumruhusu Mo J awe anakuja kumuona mtoto kwani licha ya yote, bado ni baba wa mtoto wake.

Gigy Money alienda mbali zaidi na kusema anampenda sana Mo J, sana kama ambavyo anampenda Mayra. Ameweka mbali chuki na sasa
 wanaangalia ustawi wa mtoto wao! SLIDE kusoma andiko lote.




from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/ZcM8uiY
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI