Washukiwa ugonjwa wa Marburg wafikia 205 Kagera


Idadi ya washukiwa wa Ugonjwa Wa Marburg Mkoani Kagera imefikia watu 205 Kutoka 193 kama ilivyokuwa imeelezwa na Mganga Mkuu wa Serikali, Prof.Tumain Nagu hapo awali Machi 23, Mwaka huu (2023).



Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu hii leo March 25, 2023 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Manispaa ya Bukoba na kusema mpaka sasa hakuna visa vipya vya wagonjwa wala kifo kilichotokea.


Amesema, “bado tuna visa nane ikiwa ni vifo vitano na wa tatu bado wanaendelea na mabibabu, lakini washukiwa waliochangamana na wagonjwa wameongezeka na kufikia 205, ambao ni wanafamilia na wataalamu wetu wa afya waliohudumia wagonjwa hao, hii ni dhahili kuwa ugonjwa huu haujatoka nje ya familia ambazo zimeathiliwa na ugonjwa huo.”


Waziri wa afya, Ummy Mwalim alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kwenye Ofisi za Mkuu wa Mkoa Kagera.

Tuungane kutokomeza Kifua Kikuu: Waziri Mkuu

Aidha, amesema watu hao waliotengwa sio wagonjwa na hawana dalili zozote ila wamezuiliwa kwa muda ili kuwalinda wenyewe endapo watapata dalili pamoja na kuilinda jamii huku akisisitiza kuwa mtu kama hana dalili za ugonjwa huo hawezi kumuambukiza mtu mgonjwa mwingine.


“Ugonjwa wa Marburg huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa majimaji ya mgojwa mwenye ugonjwa huo, mate, mkojo, damu au kinyesi kutoka kwa mtu aliyefariki kwa ugonjwa huo au mtu anayeonyesha dalili za ugonjwa wa Marburg, vilevile unaweza kutokea kwa wanyama kama vile popo na nyani kwenda kwa binadamu endapo atakula au kugusa mizoga ya wanyama hao,” amesema Waziri Ummy.


Hata hivyo, ameongeza kuwa timu ya wataalamu wabobezi wa kupambana na ugonjwa huo wameishawasili mkoani Kagera ili kusaidizana na wataalamu wengine wa afya walioko mkoani humo huku amewataka wananchi mkoani Kagera kuendelea kuchukua taadhari za kujikinga na ugonjwa huo kama wanavyoelekezwa na wataalamu wa afya ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa maji tiririka pamoja na kutumia vitakasa mikono.


Waziri Ummy amebainisha kuwa, Serikali kwa kushirikiana na wataalamu wa afya wanaendelea kupambana na ugonjwa huo kwa kuanza kupima joto la wasafiri wote wanaoingia na kutoka nje ya Mkoa wa Kagera, huku akiwataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kuwaingizia kipato.


Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani -WHO, Zabron Yoti amesema juhudi zinazofanywa kudhibiti ugonjwa huo kwasasa ikiwa ni siku tisa tu tangu utangazwe na ukiwa navisa vichache, ni kwa ajili ya kuzuia mapema usisambae maeneo mengine.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/ah9FBjG
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI