Bondia Mwakinyo Ataja Kikwazo KO



BONDIA Hassan Mwakinyo amesema sababu ya kutokumpiga kwa KO, Muvesa Katembo wa Afrika Kusini ni kutokana na bukta yake kumbana.

Katika pambano hilo lilofanyika juzi katika Uwanja wa Jamhuri Jijini hapa, Mwakinyo alishinda kwa pointi ambapo jaji namba moja alimpa pointi 77-74, wa pili 76-75 na watatu 77-74.

Mara ya mwisho kwa Mwakinyo kuingia ulingoni ilikuwa Septemba 3, mwaka jana ambapo alipambana na bondia Liam Smith mjini Liverpool na kupoteza kwa TKO katika raundi ya nne.

Mwakinyo aliyewahi kuingia kwenye 20 bora ya dunia kwenye uzani wa superwelter na namba moja nchini kwenye kila uzani ‘pound for pound’ ameporomoka kote na sasa ni wa pili nchini na wa 66 duniani.


Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Mwakinyo alisema sababu ya kutopata matokeo mapema na kushindwa kupata TKO ni kutokana na bukta kumbana.

"Bukta ilikuwa inaninyima uhuru wa kunyanyua mguu, kikubwa nashukuru nimeshinda, nawashukuru mashabiki wamejitokeza kwa wingi licha ya mvua iliyokuwa ikinyesha," alisema Mwakinyo.

Alisema baada ya ushindi huo anajiandaa kwa mchezo unaofuata ambapo atapanda ulingoni Juni 24, mwaka huu kucheza na bondia mkubwa ambaye hakumtaja jina.


Kwa upande wake, Katembo alisema Mwakinyo ni bondia mzuri na ameyakubali matokeo hayo huku akilalamika sehemu ya kuchezea ilikuwa ikiteleza.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/KiFcyu7
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI