Hitilafu za Umeme Katika Uwanja wa Benjamin Mkapa..Hii ni Mara ya Pili


Hitilafu za umeme katika Uwanja wa Benjamin Mkapa zimeendelea ambapo leo tena zimesimamisha mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji Yanga dhidi ya Rivers United.

Mchezo huo ulisimama dakika ya 25 kipindi cha kwanza zikianza kuzimika Moja kwenda nyingine kisha kumalizika zote zinazozunguka uwanja huo.

Baada ya kuzimika kwa taa hizo mwamuzi wa mchezo huo Jiyed Redouane kutoka Morocco alisimamisha mchezo na timu kubaki uwanjani zikisubiri kuwaka tena kwa taa hizo.

Hata hivyo baada ya dakika 6 baadaye zilianza kuwaka taratibu Moja na kuondoa giza kubwa lililokuwa uwanjani.

Jiyed ilipotimu dakika 40 ambapo ni dakika 15 baadaye tangu zilipozimika alizirudisha timu vyumbani huku taa hizo zikiendelea kuongezeka kuwaka.

Dakika nane baadaye mwamuzi huyo alirudi uwanjani huku taa zikiendelea kuwaka ambapo pia dakika Moja baadaye wenyeji Yanga pia walirejea na kuanza kupasha misuli na kufuatiwa na Rivers.

Hii ni mara ya pili kwa taa hizo kuzimika wakati mchezo unaendelea ambapo mara ya mwisho zilizimika wakati timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ikicheza dhidi ya Uganda kuwania kucheza Fainali za Mataifa Afrika.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/3cm01OA
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI