Jean Baleke Aichimba Mkwara Wydad AC "Nitawafunga Tena"



Mshambuliaji kutoka DR Congo Jean Othos Baleke amesema Simba SC ina nafasi kubwa ya kutinga Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa kuitoa Wydad AC.

Simba SC itacheza ugenini mchezo wa Mkondo wa Pili wa Robo Fainali Jumamosi (April 29) katika Uwanja wa Mohammed V, ambao upo mjini Casablanca nchini Morocco, huku ikiwa na mtaji wa bao 1-0 baada ya kushinda mchezo wa Mkondo wa Kwanza Jumamosi (April 22) Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Baleke ambaye alifunga bao la ushindi katika mchezo dhidi ya Wydad AC amesema kwa sasa wanajiandaa na mchezo wa marudiano, na wana matarajio makubwa ya kupata ushindi utakaowapeleka Nusu Fainali.

“Malengo yetu ni kufika Nusu Fainali, tunawaheshimu Wydad ni miongoni mwa timu bora na ngumu lakini tuko tayari kupambana, jambo zuri ni kuwa tunarudi tena Morocco na mchezo wa mwisho tulicheza dhidi ya Raja Casablanca pale nami nilifunga bao moja.”


“Kuhusu maandalizi hilo ni swala lililo chini ya kocha mkuu na tutasubiri kuona namna gani ataiandaa hiyo mechi lakini ukweli ni kwamba tuna nafasi kubwa ya kufanya vizuri na kupata matokeo yatakayotupeleka nusu fainali.” amesema Baleke

Simba SC inatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam Alhamis (April 27) kuelea Morocco tayari kwa mchezo wa Mkondo wa Pili ambao utamtoa mshindi wa jumla atakayecheza Nusu Fainali.

Simba SC itapaswa kulinda ushindi wake wa 1-0 pamoja na kusaka ushindi mwingine, huku wenyeji wao Wydad AC ikihitaji mabao 2-0 ama zaidi ili kujihakikishia nafasi ya kucheza Nusu Fainali.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/yEf67Nd
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI