Mochari ya Hospitali ya Malindi Yalemewa na Miili ya Mateka wa Pasta Mackenzie



Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Kilifi- Malindi imeshuhudia ongezeko la miili ya wafuasi wa dhehebu tata ya pasta Paul mackenzie.



Mochari ya Hospitali ya Malindi Yalemewa na Miili ya Mateka wa Pasta Mackenzie. Chanzo: UGC
Kutokea kwa familia za waathiriwa kutafuta miili ya wapendwa wao huku wapelelezi wakiendelea kufukua miili zaidi na kupeleka hospitalini, imedumisha harufu ya kifo na uchungu.

Robert Chonga, afisa anayesimamia hospitali ya kaunti ndogo ya Malindi, amefichua kuwa chumba cha kuhifadhia maiti kimezidiwa na idadi ya miili kutoka msitu wa Shakahola.


Chonga alieleza kuwa wanatafuta njia mbadala ya kuhifadhi miili iliyofukuliwa kwa heshima ya maiti.

"Hii mortuary kwa kweli imelemewa. Hata hivi tutapata njia mbadala ya kuweza kuhifadhi zile miili. Tunaangalia njia kadhaa kueza kuona njia mwafaka ya kuweka hii miili kwa njia ambayo inaonyesha heshima," Chonga alisema.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/tCwn7SV
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI