Rais amuagiza Katibu kuuza magari yote ya kifahari

 


Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema amemuagiza Katibu wa Baraza la Mawaziri nchini humo, Patrick Kangwa kuuza magari yote ya kifahari yaliyonunuliwa kwa ajili ya Maofisa Wakuu wa Serikali wakati wa utawala wa UPND.


Hatua hiyo, inatokana na kiapo cha utawala wake cha kuzuia ubadhirifu wa maafisa wa Serikali, jambo ambalo lilidhihirika katika utawala uliopita, huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia kiapo hicho na kwamba magari hayo ya kifahari hayana ulazima.


Aidha, Rais Hichilema amesisitiza pia dhamira ya Serikali yake ya kuwatumikia watu wa Zambia na kusimamia uwajibikaji wa maofisa walioteuliwa na agizo lake ni sehemu ya juhudi za utawala wake kupunguza matumizi ya serikali na kudhibiti ufisadi.


Hata hivyo, ameonesha kusikitishwa na kitendo cha baadhi ya Mawaziri na Makatibu Wakuu kushindwa kutekeleza majukumu yao na badala yake kuendekeza starehe na kushinda mtandaoni huku akiwataka wahakikisha wanafanisha lengo la kisera na programu za serikali kiufasaha.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/SVmdiPD
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI