Rivers United Wavamiwa Dar, Basi Lao Lapuliziwa sumu, Waiba Dola Elfu 5

 


Rivers United Wavamiwa Dar, Basi Lao Lapuliziwa sumu, Waiba Dola Elfu 5

Klabu ya soka ya Rivers United kupitia ukurasa wao rasmi wa Twitter wametoa taarifa ya madai ya basi lao kupuliziwa kemikali ya sumu pamoja na kuibiwa fedha zilizoachwa humo wakati ndani ya uwanja kwa mazoezi usiku wa jana.


Kupitia ukurasa wao wa Twitter Rivers wameandika;


ikiwa ni karibia masaa 24 kabla ya mchezo wa robo fainali ya kombe la shirikisho Afrika raundi ya pili ndani ya Dar es Salaam basi la Rivers United limevamiwa na vitu vyenye thamani ya maelfu ya dola za kimarekani vimeibiwa "


" Rivers United imeiandikia CAF na inasubiri kuchukuliwa kwa hatua zaidi "


" waliokuwepo kushuhudia tukio hilo ni pamoja na mratibu mkuu wa CAF, Ali Nwebe kutoka Uganda na Mkuu wa Idara ya Ulinzi WA CAF, Jamil Bawalaggana Mpagi kutoka Uganda ambaye ndiye amethibitisha kuwa kemikali iliyopulizwa ndani ya basi ni sumu "


" hayo yamegunduliwa baada ya timu kumaliza mazoezi yake ya mwisho kuelekea mchezo wake dhidi ya Yanga ya Tanzania ndipo ilipojulikana kuwa basi la timu limeingiliwa na kupuliziwa kemikali ya sumu pamoja na kuibiwa jumla ya USD 5,250 "



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/BRXo8Zl
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI