Wababe Wanne Waliotinga Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa

 

Wababe Wanne Waliotinga Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa


Mechi mbili za robo fainali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika zilihitimishwa usiku wkuamkia leo kwa mabingwa wa kihistoria Al Ahly kukata tiketi kibabe baada ya kulazmisha suluhu ya bila kufungana nchini Morocco dhidi ya Raja Casablanca

Al Ahly walishinda mabao 2-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa huko Misri

Al Ahly iliungana na Esperance ya Tunisia ambayo pia ilitinga nusu fainali licha ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya JS Kbalylie

Esperance ilishinda bao 1-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Algeria

Mapema jana Mamelodi Sundowns ilitinga nusu fainali kibabe kwa ushindi wa jumla wa mabao 6-2 dhidi ya CR Belouizdad

Mamelod walishinda mabao 2-1 katika mchezo wa mkondo wa pili wakiongezea juu ya ushindi wao wa mabao 4-1 katika mchezo mkondo wa kwanza

Al Ahly, Mamelod na Esperance zimeungana na Wydad Athletic ambayo ilitangulia nusu fainali juzi kwa ushindi wa mikwaju ya penati dhidi ya Simba ya Tanzania baada ya marokeo ya sare ya bao 1-1 katika mechi zote mbili za robo fainali

Al Ahly itachuana na Esperance hatua ya nusu fainali wakati Mamelodi watachuana na wydad Athletic



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/j9CWxJY
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI