Askari Wawili Wauawa Mbuga ya Wanyama

 


Walinzi wawili wa Mbuga za Wanyama Virunga, wameuawa na wengine sita kujeruhiwa katika shambulio jipya la eneo la mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC.

Katika taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Mbuga hiyo, imesema washambuliaji hao wanaaminika kuwa ni wapiganaji wa kundi la Mai Mai Kabido au Wanamgambo wa jamii ambao wawindaji na ni miongoni mwa makumi ya makundi yanayoendesha mashambulizi eneo la mashariki mwa DRC.

Aidha, taarifa hiyo imesema wakati wa doria katika mbuga hiyo karibu na mwambao wa Ziwa Edward ambalo lililopo mpakani mwa Uganda, walinzi hao wawili wa mazingira walifariki baada ya kupigwa risasi na kutokana na majeraha waliyoyapata.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Afisa wa kituo cha Vitshumbi, kijiji cha wavuvi kilichopo Vitshumbi, Kambale Muhindo alisema, “tulisikia milio ya risasi kundi la wawindaji haramu waliua kiboko na ili kujilinda waliwavizia walinzi wa mbuga hiyo.”



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/uNlGzVZ
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI