Mshambulizi Wa Man City Ashinda Tuzo Ya Mchezaji Bora Chipukizi Wa EPL

Mshambulizi Wa Man City Ashinda Tuzo Ya Mchezaji Bora Chipukizi Wa EPL


Mchezaji wa Manchester City Erling Haaland amekuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo za mchezaji bora wa mwaka wa Primia Ligi katika msimu mmoja.

Mabao 36 ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 yamemfanya avunje rekodi ya Ligi Kuu ya England ya kufunga mabao mengi zaidi kwa msimu mmoja.

Kwa jumla, amefunga mabao 52 wakati wa shindano.

“Nina heshima kuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo zote mbili katika msimu mmoja – asante kwa kila mtu aliyenipigia kura,” alisema Haaland.

Haaland, ambaye alipata kura nyingi zaidi kutoka kwa umma na jopo la Primia Ligi, alijiunga na City kutoka Borussia Dortmund msimu uliopita na ameisaidia klabu hiyo kushinda taji la tatu mfululizo la ligi ya juu.

Tayari ameteuliwa kuwa Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Soka (FWA)

“Umekuwa msimu wa kwanza wa ajabu katika Ligi Kuu na kunyanyua kombe wikendi iliyopita mbele ya mashabiki wetu pale Etihad ulikuwa wakati wa kipekee sana kwangu,” aliongeza mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway.

City pia wako mbioni kuwania Treble kwani watamenyana na Manchester United katika fainali ya Kombe la FA mnamo 3 Juni kabla ya kucheza na Inter Milan katika fainali ya Ligi ya Mabingwa mnamo Juni 10.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Akab1qC
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI