Polisi Mkoa wa Arusha Wamkamata Aliyemtoa Meno Mkewe kwa bisi bisi


Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha, limemkamata Isack Robertson (45) mkazi wa Sombetini Jijini Arusha kwa tuhuma za kumpiga, kumng'oa meno na kumtoboa macho mke wake Jackline Mkonyi (38).Mwanaume huyo amekamatwa Mei 27, 2023, maeneo ya Himo mkoani Kilimanjaro akiwa amejificha kwa Mchungaji.
Taarifa hiyo imetolewa leo Mei 28, 2023, na Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo, na kusema mtuhumiwa wanaendelea kumhoji na pindi upelelezi utakapokamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.

Aidha ametoa onyo kwa baadhi ya watu wachache wanaofanya vitendo vya ukatili katika familia zao ama sehemu nyingine kuacha mara moja kwani hawatasita kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria.

Lakini pia amewaomba wananchi popote walipo wasifumbie macho vitendo viovu na waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha wanatoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika maeneo yao ili kukomesha matukio hayo katika jamii.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/rLGEYJa
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI