Sheria Inayombana Ally Kamwe Baada ya Kumtukana Juma Mgunda Hadharani


Kupitia sheria na kanuni zilizowekwa za Bodi ya Ligi kuhusu udhibiti wa viongozi huenda Afisa Habari wa klabu ya Young Africans Ali Kamwe akafungiwa miezi mitatu kujihusisha na soka, endapo sheria zitafutwa baada ya kumfananisha Kocha Msaidizi wa Simba SC Juma Mgunda na Andazi mbele ya Mashabiki wa Young Africans.

Kwa mujibu wa Kanuni nambari 46 : udhibiti wa viongozi kifungu nambari 8 kinamfunga Ally Kamwe kwa maneno wa kashfa na dhihaka kwa Juma Mgunda, na mbaya zaidi aliyatoa hadharani na kunukuliwa na vyombo vya habari.

Kanuno hiyo inasema: “Kiongozi Akitoa matamshi au ishara za matusi dhidi ya mashabiki, akitoa matamshi, ishara za matusi yenye nia ya kumdhalilisha kiongozi mbele ya jamii awe wa TFF, Klabu au Taifa atatozwa faini ya shilingi milioni moja 1,000,000/- na kufungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu (3).

Kanuni nambari 47 : udhibiti wa klabu, nayo inambana Ally kamwe kwa kauli aliyoitoa jana Ijumaa (Mei 26) inayosema: “Klabu ina wajibu na jukumu la kuhakikisha kuwa wachezaji, viongozi, wanachama na wapenzi wake wanajiheshimu na hawajihusishi na vitendo vyovyote vya utovu wa nidhamu kama vile matusi, vitisho, vurugu, vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina na vitendo vyovyote vingine visivyokuwa vya kimichezo kwenye viwanja vya michezo. Klabu ambayo mashabiki/wachezaji/viongozi wake watafanya vitendo hivyo itatozwa faini ya shilingi Milioni moja (1,000,000/-).”

Hata hivyo pamoja na kanuni hizi kueleza namna ambavyo kiongozi ambaye ni mwanafamilia ya Soka nchini Tanzania anavyotakiwa kuadhibiwa akikutwa na hatia, bado Mamlaka za soka zitapaswa kutoa maamuzi kama itaonekana inafaa dhidi ya Ally Kamwe.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/BMSRHwl
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI