Breaking: Waliokuwa Kwenye Chombo Kilichopotea Baharini Wakienda Kuangalia Mabaki ya Titanic Wote Wamefariki Dunia



Taarifa ya muda huu inaeleza kuwa watu wote watano (5) waliokuwa kwenye meli ya chini ya maji (Monawari) iliyotoweka walipokuwa wakijaribu kutalii kwenye mabaki ya Meli ya Titanic wamekufa.

Taarifa kutoka kampuni ya OceanGate Inc. Inayomiliki kifaa hicho (Monawari) imesema kuwa “Sasa tunaamini kwamba Mkurugenzi Mtendaji wetu Stockton Rush, Shahzada Dawood na mwanawe Suleman Dawood, Hamish Harding, na Paul-Henri Nargeolet, wamepotea. Wanaume hawa walikuwa wagunduzi wa kweli ambao walishiriki ari tofauti ya matukio, na shauku kubwa ya kuchunguza na kufanya utalii wa bahari za dunia. Mioyo yetu iko pamoja na nafsi hizi tano na kila mwanafamilia katika kipindi hiki cha msiba. Tunasikitika kwa kuwapoteza wapendwa wetu.

Tangazo hili la vifo vya watu hao watano linakuja saa chache baada baadhi ya sehemu za chombo hiko (Monawari) kuonekana karibu na mabaki ya Titanic siku ya Alhamisi, na wataalam haraka walifanya kazi ya kutathmini walichokipata ... huku rafiki wa watu 2 kati ya waliopotea akidai ilikuwa fremu ya kutua na kifuniko cha nyuma cha chombo.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/DfB92cS
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI