Mabaki ya Waliofariki Kwenye Nyambizi Haiwezi Kupatikana



Sehemu ya mabaki ya Submarine hiyo ya Titan imegunduliwa ndani ya eneo la utafutaji na roboti ya ROV karibu na mabaki ya meli ya Titanic, Walinzi wa Pwani wa Marekani wametangaza hivi punde.

Wataalam kwasasa wanatathmini habari hiyo.

Taarifa kutoka kwa walinzi wa pwani inasema kwamba roboti aina ya ROV imepata mabaki katika sakafu ya bahari karibu na mabaki ya meli ya Titanic .

Admirali John Mauger anayeongoza utafutaji huo pamoja na na kamanda Jamie Frederick wamezungumza katika kikao ma wanahabari.

Maafisa wanasema vipande vitano vikubwa vilipatikana pamoja na mabaki karibu na meli ya Titanic. Miongoni mwao , ni pamoja na pua ya nyambizi hiyo.(muonekano wa mbele)

Admiral Mauger anasema hawezi kuthibitisha kama Walinzi wa Pwani wa Marekani wataweza kuipata miili ya abiria watano waliokuwemo ndani ya nyambizi ndogo ya Titan.

Ingawa bado wanaendelea kuyatafuta mabaki yote na kuona kama wataipata miili hiyo au laaah


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/nABhJOV
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI